Steinmeier Indonesia | Matukio ya Kisiasa | DW | 27.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Steinmeier Indonesia

Waziri wa nje wa Ujerumani anatembelea Indonesia na alikua leo na mazungumzo na waziri mwenzake wa nchi hiyo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier (kushoto) na mwenyeji wake wa Indonesia Hassan Wirajuda

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier (kushoto) na mwenyeji wake wa Indonesia Hassan Wirajuda

Waziri wa nje wa Ujerumani Bw.Frank-Walter Steinmeier, akiendelea na ziara yake nchini Indonesia, alikuwa na mazungumzo leo na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Indonesia-nchi yenye wakaazi wengi kabisa wa kiislamu ulimwenguni.Katika shina la mazungumzo yake na mwenzake Hassan Wirajuda ,waliutaka utawala wa kijeshi wa Burma au Myanmar kufungua mlango wazi kwa demokrasia.

Bw.Steinmeier anatembelea leo shule ya kijerumani ilioasisiwa mjini Djakarta tangu miaka 50 iliopita.

Baada ya mazungumzo yake leo na waziri wan je wa Indonesia Hassan Wirajuda, waziri wan je wa Ujerumani alitangaza kuundwa kwa kikundi cha mabingwa kutoka nchi zote mbili ili kuendeleza mbele mazungumzo kati ya dini mbali mbali.

Kwani, Indonesia ikiwa na wakaazi milioni 240 ndio taifa lenye wakaazi wengi kabisa wa kiislamu duniani.

Jana waziri wan je wa Ujerumani,alikutana na waakilishi wa dini mbali mbali huko Indonesia.Akapongeza baadae juu ya uislamu usiofuata itikadi kali katika dola hili kuu la kiislamu duniani.

Akitoa mfano wa kuishi pamoja kwa mila na tamaduni mbali mbali nchini Indonesia , Bw.walter-Steinmeier alitaja shule ya kijerumani ilioanzishwa Djakarta, miaka 50 nyuma.

Bw.Steinmeier akatangaza kutanuliwa zaidi shule za kijerumani nchi za n’gambo ili kutilia nguvu utamaduni wake zaidi kuliko hadi sasa.

Ujerumani na jumla ya shule zake 117 katika nchi 63 mbali mbali na hadi shule 400 nchi za nje zenye tawi la kijerumani.Mfumo huo anapanga sasa waziri Steinmeier anapanga sasa kuutanua kwa kuanzisha ushirika wa shule .Ukilinganisha na Ujerumani, Ufaransa ina shule zake 252 ngambo katika nchi 252.

Katika jukwaa la kisiasa, waziri wan je wa Ujerumani na mwenzake wa Indonesia Wirajuda, waliitaka serikali ya kijeshi ya Myanmar au Burma, kutekeleza nchini demokrasia tena bila kigeugeu.

Wirajuda alikaribisha mikono miwili tangazo la Myanmar la kuifanyia mageuzi katiba yake pamoja na azma yake ya kuitisha uchaguzi mkuu 2010.

Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Myanmar kutangaza mpango na wakati wa kuirejesha Myanmar katika mkondo wa demolkrasia na lini.

Bw.Steinmeier aliipongeza Indonesia kwa hatua ilizopiga tangu kumalizika kwa enzi ya utawala wa dikteta Jamadari Suharto kiasi cha miaka 10 iliopita.Akasema na ninamnukulu:

“Ujerumani inaangalia hatua hizo kwa heshima kubwa na inaziungamkono kwa uwezo wake wote.”-alisema Frabk Walter-Steinmeier.

Akitupia macho juhudi za ulinzi wa mazingira,Bw.steinmier ameungamkono juhudi za kukuuza upya misitu nchini Indonesia .Ujerumani inachangia Euro milioni 24 katika mradi huo mbali na Euro milioni 60 zinazotoka Banki kuu ya dunia.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com