Somalia: Rais atia saini sheria ya kurefusha muda wake uongozini | Matukio ya Afrika | DW | 14.04.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Somalia: Rais atia saini sheria ya kurefusha muda wake uongozini

Rais wa Somalia ametia saini na kuwa sheria muswada wa kuendelea kusalia madarakani pamoja na serikali yake, wakati Marekani na mataifa mengine yakitishia kuiwekea vikwazo nchi hiyo iliyogubikwa na machafuko.

Mvutano huo unaongeza mgogoro wa kisiasa wa miezi kadhaa baada ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari kucheleweshwa. Wakosoaji wanasema muda wa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed kusalia madarakani umemalizika.

Jamii ya kimataifa ilipinga sheria hiyo ya Rais Mohamed kuendelea kusalia madarakani, na imeonya kuwa kundi la kigaidi la Al-Shabab huenda likatumia mwanya huo wa mgawanyiko wa kisiasa kufanya mashambulizi.

soma zaidi: UN yawahimiza viongozi Somalia kuafikiana juu ya uchaguzi

Jana Jumanne, Rais huyo alitia saini sheria tata baada ya bunge nchini humo mapema wiki hii kupiga kura ya kuendelea kusalia madarakani kwa miaka miwili zaidi.

Hata hivyo, viongozi wa baraza la Seneti la nchi hiyo wamesema kura hiyo haramu.