Sio suluhisho lakini ni maendeleo | Matukio ya Kisiasa | DW | 18.05.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Sio suluhisho lakini ni maendeleo

Iran sasa ipo tayari kurutubisha madini yake ya uranium katika nchi ya nje. na siku ya Jumatatu, makubaliano hayo yalitiwa saini pamoja na Uturuki na Brazil.

MVom Rechts der türkische Regierungschef Recep Tayyip Erdogan, der iranische Präsident Mahmud Ahmadinedschad, der iranische Außenminister Manoutschehr Mottaki, und der brasilianische Staatspräsident Luiz Inácio Lula da Silva in Teheran / Iran nach dem Unterzeichnen des Austauschabkommen 17.05.2010

Kuanzia kulia-Waziri Mkuu wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan,Rais wa Iran Mahmud Ahmadinejad, Waziri wa Nje wa Iran Manouchehr Mottaki na Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva.

Ikiwa baadhi ya wataalamu wataaminiwa basi mtu atadhani kuwa mgogoro wa mradi wa nyuklia wa Iran umepatiwa ufumbuzi. Kila mmoja anagependa kuona hilo lakini ukweli ni tofauti, kwani mara nyingine tena Iran imeeleza wazi wazi kuwa haitorotubisha madini yake yote ya Uranium katika nchi ya nje, bali ile itakayotumiwa katika mradi wake mmoja tu.

Kuambatana na makubaliano yaliyotiwa saini, kiasi ya tani 1.2 ya madini ya Uranium yaliyorutubishwa kwa kiwango cha chini, yatasafirishwa Uturuki. Mwaka mmoja baadae, Iran itapokea kilo 120 za uranium iliyosafishwa kwa kiwango cha asilimia 20. Hiyo itakuwa chini ya usimamizi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia IAEA. Hiyo humaanisha kuwa mitambo ya kurutubisha uranium, itaendelea kufanya kazi nchini Iran. Kwa hivyo, nchi za Magharibi hazitokosea, kuuliza ikiwa mradi wa nyuklia wa Iran ni kwa matumizi ya amani tu au ya kijeshi.

Hata ikiwa ni machache tu yaliyokidhiwa kuliko wengine wangependelea kuona katika makubaliano hayo, ukweli ni kwamba kumechukuliwa hatua kadhaa. Kwanza, ni kuwa Iran imeonyesha kuwa ipo tayari kufanya majadiliano,hata ikiwa kulihitajiwa subra kubwa na vitisho kadhaa. Hata hivyo, Iran imesalim amri na imekubali pendekezo la kupatanisha lililotolewa na Uturuki na Brazil. Na hilo ni la kufuarahia.

Pili, ni ukweli kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeitikia mwito wa Uturuki na Brazil. Kwa kukubali kufanya majadiliano hayo kupitia nchi hizo zinazoinukia kiuchumi,Iran imepandisha hadhi ya nchi hizo mbili na imeyapuuza mataifa ya magharibi yalio na kura turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Vile vile, Iran imejitoa katika hali ya kutengwa kimataifa. Kwa hivyo, nchini Iran Rais Mahmoud Ahmadinejad anaweza kujisifu kuwa wameibuka na ushindi.

Tatu, ni kwamba Iran, bado inakabiliwa na vikwazo vipya vilivyopendekezwa na Marekani na washirika wake, kwani nchi hiyo bado haijaweka wazi mradi wake wa nyuklia. Hata hivyo, itakuwa busara kwa nchi za Magharibi kuacha kutishia kuweka vikwazo vipya. Rais Ahmedinejad ambae jana Jumatatu alisema, majadiliano mapya yanapaswa kufanywa pamoja na mataifa yenye kura turufu na Ujerumani, kwa sasa anaweza kuaminiwa. Kwa namna hiyo inapatikana njia ya kuketi pamoja na kujadiliana.

Mwandishi:Pick/Ulrich/ZPR

Mhariri:M.Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com