1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la Chakula Duniani WFP lashinda Tuzo ya Amani, Nobel

Iddi Ssessanga
9 Oktoba 2020

Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa WFP limeshinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu kutokana na juhudi zake za kupambana na nja, kuboresha mazingira ya mizozo, na kuzuwia matumizi ya njaa kama zana za kivita na mzozo.

https://p.dw.com/p/3jfwJ
Logo Welternährungsprogramm der Vereinten Nationen

Ikitangaza uamuzi wake, kamati ya Nobel imesema imelenga kugeuza jicho la dunia kwa mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa na umaskini wa chakula. 

Tangazo hilo limetolewa mjini Oslo na Berit Reiss-Andersesn, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Nobel. Kamati hiyo imesema janga la virusi vya corona limeongezea tatizo la njaa linalowakabilia mamilioni ya watu kote duniani, na kuzitolea wito serikali kuhakikisha kwamba WFP na mashirika mengine ya msaada yanapokea msaada wa kifedha unaohitajika kulisha watu hao.

Kamati ya Nobel ya Norway, imeamua kutoa tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka 2020 kwa shirika la chakula duniani, kutokana na juhudi zake za kupambana na nja, na mchango wake katika kuoberesha mazingira kwa ajili ya amani katik maeneo yalioathiriwa na mizozo, na kwa kuongoza juhudi za kuzuwia matumizi ya njaa kama zana ya kivita na mzozo.

Shirika hilo la mpango wa chakula duniani limetuzwa kutokana na mchango wake wa kupambana na njaa ulimwenguni.
Shirika hilo la mpango wa chakula duniani limetuzwa kutokana na mchango wake wa kupambana na njaa ulimwenguni.Picha: Maciej Moskwa/NurPhoto/picture-alliance

Reiss-Anderesen amesema WFP inachangia kila siku katika kuendeleza udugu wa mataifa yaliotajwa ktik wasia wa Alfred Nobel. Hakukuwa na uhabada wa sababu au wagombea kwenye orodha ya mwaka huu, ambapo watu 211, mashirika 107  waliteuliwa kuelekea muda wa mwiso wa Faebruari Mosi.

Hata hivyo, Kamati ya Nobel ya Norway, inabakiza usiri wa juu kabisa kuhusu nani inampendelea kwa tuzo hiyo ya heshima zaidi duniani. Tuzo hiyo inaambatana na zawadi ya pesa taslimu kiasi cha dola milioni 1.1 pamoja na medali ya dhahabu vinavyotolewa katik sherehe mjini Oslo, Norway, Desemba 10, ambayo ndiyo tarehe ya kukumbuka kifo cha Alfred Nobel. Sherehe ya mwaka huu ilipunguzwa ukubwa kutokana janga la virusi vya corona.

Baadhi ya waathiriwa wa njaa wakipokea chakula cha misaada cha kila mwezi kutoka katika shirika la WFP jimbo la Cabo nchini Msumbiji Agosti 27, 2020.
Baadhi ya waathiriwa wa njaa wakipokea chakula cha misaada cha kila mwezi kutoka katika shirika la WFP jimbo la Cabo nchini Msumbiji Agosti 27, 2020.Picha: Falume Bachir/World Food Program/AP/picture-alliance

Msemaji wa WFP, Tomson Phiri, amesema ni jambo la fahari kwa shirika hilo kutambuliwa na tuzo hiyo, na kusema hata kuteuliwa tu kuwa kwenye orodha hilo lilikuwa jambo tosha, lakini ushindi ni jambo la kusisimuwa zaidi.

Tomson amezungumzia kazi ya shirika kutoa chakula na ugavi mwingine wakati wa janga la covid-19 wakati ambapo mashirika ya ndege hayakuwa yanafanyakazi tena, na kusema kwamba ilikwenda mbali zaidi ya wito. WFP ndiyo shirika kubwa zaidi la misaada linaloshughulikia njaa na kuendeleza ukuzaji wa usalama wa chakula duniani.