Shelly-Ann Fraser-Pryce achukua dhahabu | Michezo | DW | 25.08.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Shelly-Ann Fraser-Pryce achukua dhahabu

Mwanariadha wa Jamaica Shelly-Ann Fraser-Pryce alitimka kwa kasi na kutwaa medali ya dhahabu katika mbio za mita 100 kwa upande wa wanawake kwenye mashindano ya riadha ya dunia yanayoendelea Beijing, China

Ilikuwa ni dhahabu ya sita kwa mwanariadha huyo kushinda baada ya kushinda mbio za mita 100 na 200 mwaka 2013.

Schippers ni bingwa wa mbio za Heptathlon baada ya kushinda medali ya shaba miaka miwili iliopita.

Ni rekodi ya taifa kwa upande wa Schippers ambaye alianza kushiriki katika mbio fupi mnamo mwezi Juni huku Bowie mwenye umri wa miaka 24 akinyakua taji lake kuu la kwanza.

Mwanariadha wa Nigeria aliyepigiwa upatu kufanya vizuri Blessing Ogakbare alishika mkia katika mbio hizo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Sekione Kitojo