Shambulizi la Urusi nchini Ukraine lawajeruhi watu 11
31 Oktoba 2025
Matangazo
Kupitia ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa Telegraph, kitengo hicho cha huduma za dharura kimesema shambulizi hilo la Urusi lililenga jengo la makazi la ghorofa, nyumba binafsi pamoja na miundombinu.
Gavana wa eneo hilo Ihor Kalchenko, amesema Urusi ilikuwa imeshambulia pia karakana ya reli na kuharibu mabehewa kadhaa na majengo.
Eneo hilo la Sumy linapakana na Urusi na limekuwa chini ya mashambulizi ya mara kwa mara ya droni na makombora.