Serikali ya Burundi yaanza msako wa usalama | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Serikali ya Burundi yaanza msako wa usalama

Zoezi la kuwapokonya silaha kwa nguvu watu wanaozimiliki kinyume cha sheria,lilizinduliwa rasmi jana mjini Bujumbura, Burundi. Wakati zoezi hilo likifanyika raia wa 3 wameuwawa katika mtaa wa Musaga.

Ikiwa ni siku ya pili leo ya zoezi hilo la kuwapokonya silaha kwa nguvu watu wanaozimiliki kinyume cha sheria, zoezi hilo linafanyika katika mtaa wa Musaga kusini mwa jiji la Bujumbura. Hata hivyo kumeripotiwa makabiliano ambapo raia watatu wameuwawa huku miripuko ya guruneti ikiendeleakusikika. Miili ya watu hao imeondolewa katika mtaa huo na wafanyakazi wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu.

Barabara kuu zinazoingia Musaga zimeonekana kufurika walinda usalama. Ni katika mtaa wa Mutakura uliyo kaskazini mwa jiji la Bujumbura, kunakoshuhudiwa pia usalama mdogo tangu ulipo zuka mzozo wa sasa Burundi,ndipo lilipo zinduliwa zoezi hilo la kuwapokonya silaha kwa nguvu wanaozimiliki kinyume cha sheria. Nyumba hadi nyumba wakiwa na vifaa mbalimbali vya kijeshi walinda usalama wa kikosi maalumu cha ulinzi wa rais ndio wanao tekeleza Operesheni hiyo.

Wengi wakimbia makazi yao

Waziri wa usalama Alain Guillaume Bunyoni amesema, baada ya kumalizika muda wa ziada uliokuwa umetolewa na rais, wanahakikisha ya kuwa hakuna silaha zinazo endelea kumilikiwa na raia kinyume cha sheria.

Miongoni mwa walioyapa kisogo makaazi yao katika mitaa hiyo si raia wa kawaida pekee, bali pia viongozi wa china na madiwani na wabunge wote wakihofia usalama wao. Waziri Bunyoni amesema msako huo unafanyika kitaalamu na walinda usalama hawatoondoka hadi pale usalama utakapokuwa umerejea katika mitaa hiyo.

Zoezi hilo la kuwapokonya silaha kwa nguvu wanaozimiliki kinyume cha
sheria, linafanyika wakati ujumbe wa waangalizi wa kijeshi wa Umoja wa Afrika tayari umeingia Burundi, ambao baada ya kukutana kwa mazungumzo na waziri wa usalama ulitakiwa kufuatilia zoezi hilo linavyo endelea.


Mwandishi: Amida Issa

Mhariri:Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com