Seneta Barack Obama atamba kisiasa | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 07.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Seneta Barack Obama atamba kisiasa

---

MANCHESTER

Kura za maoni zlizofanywa na mashirika mawili tofauti nchini Marekani zinaonyesha kwamba Barack Obama anaongoza dhidi ya mpinzani wake katika chama cha Demokratic Hillary Clinton kwenye hatua za mwanzo za kuelekea uteuzi wa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho .Kura hizo za maoni zimetolewa siku moja kabla ya hapo kesho kufanyika uchaguzi wa mwanzo wa majimbo wa chama hicho.Seneta Barack Obama wa jimbo la Illinois anatajwa kuwa mbele na asilimia 13 dhidi ya bibi Hillary Clinton katika maoni yaliyofanywa miongoni mwa wapiga kura wa jimbo la New Hermpshire.Barack Obama pia alishinda kura za jimbo la Iowa alhamisi iliyopita na kumuweka katika nafasi nzuri kuelekea kinyang’anyiro cha kuwania uteuzi wa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Demokratic katika uchaguzi mkuu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com