1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Selfie

Picha za kujipiga kwa kutumia kamera zilianza katikati mwa miaka ya 2000 wakati tekonolojia ya digitali ikipanuka, na mitandao ya kijamii ikianza kuwa maarufu. Mfumo huu ulikuwa wa vijana lakini sasa kila mmoja anautumia

Nani ambaye hajajipiga picha kwa kutumia kamera ya kwenye simu? Hata Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alikuwa anajulikana kwa kujipiga picha akiwa na wanasiasa wenzake. Kwa kupanuka kimataifa kwa mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram na twita, picha za selfie zimezidi kuwa maarufu. Kuanzia nyota wa Holywood kwa watoa maamuzi duniani na viongozi wa dini, hakuna mwenye kinga dhidi ya selfie. Kama utambuzi wa umaarufu na matumizi makubwa ya neno hilo, kamusi ya Kiingereza ya Oxford ilijumlisha neno "Selfie" katika toleo lake la mtandaoni. Mwaka 2013 neno "Selfie" lilitajwa kuwa "neno la mwaka.'