1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Saudi Arabia na Wahouthi watafuta suluhu Yemen

Saumu Mwasimba
17 Januari 2023

Mazungumzo ya kutafuta makubaliano rasmi ya kusitisha vita Yemen yafufuliwa baada ya kushuhudiwa utulivu kwa zaidi ya miezi tisa

https://p.dw.com/p/4MIWT
Jemen Freude über die Abreise von Saleh 5. Juni 2011
Picha: picture alliance/dpa

Saudi Arabia na mahasimu wao, waasi wa Kihouthi nchini Yemen, wameufufua mchakato wa mazungumzo wakitarajia kuimarisha mpango usio rasmi wa usitishaji wa mapigano. Hatua hii inakuja ikiwa ni baada ya kushuhudiwa kipindi kirefu cha kusitishwa vita katika taifa hilo masikini kusini mwa Arabuni.

Jemen Freude über die Abreise von Saleh 5. Juni 2011
Picha: picture alliance/dpa

Kwa zaidi ya miezi tisa sasa  vita vimesitishwa nchini Yemen na hivi sasa, maafisa wa Yemen, Saudi Arabia na Umoja wa Maraifa wanasema  pande zilizokuwa vitani, Saudi Arabia na waasi wa Kihouthi wamefufua mpango wa mazungumzo yasiyokuwa ya moja kwa moja kuimarisha usitishaji huo wa vita na kutengeneza njia ya kufanyika mazungumzo kamili ya kumaliza vita  vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu  nchini Yemen.
Akitowa taarifa mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa,mjumbe maalum wa Umoja huo kuhusu Yemen,Hans Grundberg amesisitiza juu ya umuhimu wa kuendelezwa mazungumzo ya kidiplomaasia nchini Yemen.

"Nimalizie kwa kusisitiza kwamba nimetiwa moyo na kuongezeka kasi ya mazungumzo yanayofanyika. Yemen inahitaji  makubaliano yatakayohusisha mtazamo wa pamoja kwa ajili ya kupiga hatua mbele ili isirudi kwenye mapigano makubwa.

Kuna hali dhaifu ya utulivu, wakati kukiwa hakuna mpango rasmi wa kusitishwa vita tangu yalipomalizika makubaliano ya kusitisha vita yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa mwezi Oktoba.

Hali ya utulivu imekuwa ikitikiswa kufuatia mashambulizi ya Wahouthi dhidi ya vinu vya mafuta pamoja na kauli kali kutoka serikali inayotambuliwa kimataifa inayoshirikiana na Saudi Arabia ambayo inalalamika  kwamba hadi sasa haijashirikishwa kwenye mazungumzo.

Kwa maneno mengine kutokuwepo hatua yoyote iliyopigwa huenda kukasababisha kutokuwepo maelewano na kuzusha upya mapigano makubwa.

Jemen Huthi-Rebellen in Sanaa
Picha: imago images/Xinhua

Ingawa mpaka sasa inaonesha pande zote mbili zinataka kupata suluhu baada ya miaka minane ya kushuhudia vita vilivyouwa zaidi ya watu 150,000,na kuiacha Yemen ikiwa imegawanyika,imeporomoka na kukaribia kabisa kutumbukia kwenye baa la njaa,ukishuhudiwa mgogoro mkubwa kabisa wa kibinadamu nchini humo ambao haujawahi kuonekana duniani.

Saudi Arabia ilianzisha mazungumzo yasiokuwa ya moja kwa moja na waasi wa Kihouthi mnamo mwezi Septemba wakati ilipokuwa wazi kwamba makubaliano ya kusitisha vita yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa hayatorefushwa.

Oman ndiyo iliyokuwa ikisimama katikati kama  msuluhishi kwenye mazungumzo hayo.Afisa wa Umoja wa Mataifa ambaye hakutaka kutajwa jina, kutokana suala hili kuwa tete amesema hivi sasa hii ni fursa ya kumaliza vita hivyo vya muda mrefu ikiwa Saudi Arabia na waasi wa Kihouthi  watazungumza kwa nia njema na mazungumzo hayo kushirikisha wadau wengine wa Yemen.Hofu ya vita yarejea Yemen kwa kushindwa kurefusha mkataba

Kwa upande mwingine mwanadiplomasia mmoja wa Saudia amesema nchi yake imeziomba China na Urusi kuishinikiza Iran na Wahouthi kujiepusha na vita.

Na kwa upande wa Iran nayo imekuwa mara kwa mara ikifahamishwa na Wahouthi na Oman  kuhusu mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea na mpaka sasa Iran imeonesha kuunga mkono usitishaji mapigano ambao sio rasmi.

Jemen Freude über die Abreise von Saleh 5. Juni 2011
Picha: dapd

Vita vya Yemen vilianza mwaka 2014 baada ya kuuteka mji mkuu Sanaa na kuilazimisha serikali inayotambuliwa kimataifa kukimbilia Kusini na baadae ikenda uhamishoni nchini Saudi Arabia.Mwaka 2015 Saudi Arabia ikaamu kuingia vitani nchini Yemen ikiongoza muungano wa kijeshi- iliyounda pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu na nchi nyingine za kiarabu.