SANTIAGO : Pinochet afanyiwa upasuaji | Habari za Ulimwengu | DW | 04.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SANTIAGO : Pinochet afanyiwa upasuaji

Augusto Pinochet Generali wa zamani wa Chile anayeshutumiwa kwa mateso,mauaji na dhuluma nyenginezo wakati wa utawala wake wa kidikteta wa miaka 17 amepata mshutuko wa moyo hapo jana na kufanyiwa upasuaji wa dharura.

Daktari wa hospitali alikolazwa ameielezea hali ya matibabu ya dikteta huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 91 kuwa inaridhisha lakini amesema kuwa Pinochet bado yungali mgonjwa mahtuti.

Daktari huyo Juan Vergara amesema timu ya matibabu haifikirii kumfanyia operesheni nyengine kwa hivi sasa venginevyo hali yake inazidi kuwa mbaya sana.

Hapo jana alifanyiwa kaida au ada za kidini za mwisho za madhehebu ya Katoliki ambazo kwa desturi hufanywa na kasisi kwa mtu alie taabani kukaribia kufa kabla ya kufanyiwa upasuaji huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com