Salva Kiir na Riek Machar wakubaliana kuunda serikali ya muungano | Matukio ya Kisiasa | DW | 21.02.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Salva Kiir na Riek Machar wakubaliana kuunda serikali ya muungano

Salva Kiir amemteua Machar kuwa makamu wa rais wa kwanza na kulivunja baraza la mawaziri ili kuruhusu kuwepo kwa viongozi zaidi wa upinzani. Marekani imepongeza hatua ilioafikiwa mjini Juba.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar wamekubaliana kuunda serikali ya mseto ifikapo siku ya Jumamosi. Kiir amemteua Machar kuwa makamu wa rais wa kwanza na kulivunja baraza la mawaziri ili kuruhusu kuwepo kwa viongozi zaidi wa upinzani. Marekani ambayo inaunga mkono mchakato wa amani nchini humo imepongeza hatua ilioafikiwa mjini Juba.

Hatua hiyo inafuatia mkutano uliofanyika baina ya Salva Kiir na Riek Machar katika ikulu mjini Juba, mji mkuu wa Sudan kusini. Rais Kiir amesema kwamba maswala muhimu ambayo hayajasuluhishwa kama vile kugawana mamlaka baina yake na Machar yanatarajiwa kuangaziwa na kukamilishwa katika siku za usoni.

Südsudan Unterzeichnung Friedensabkommen in Juba Präsident Salva Kiir

Rais Salva Kier wa Sudan Kusini

''Tumekubaliana kuunda serikali ya umoja. Kuna mamabo machacheamabayo bado yanahitaji kusuluhishwa .lakini tutakamilisha hayo baada ya serikali ya mpito kuundwa.Lakini mamabo kama usalama wawapinzani mjini Juba yako mikononi mwangu''alisema Salva Kiir 

Riek Machar amekubali kuchukuwa wadhifa wake kama makamu wa rais wa kwanza. Kuundwa kwa serikali ya muungano ilikuwa nukta muhimu ya makubaliano ya amani baina ya Kiir na Machar ya mwaka 2018. Tuhuma za kwamba Riek Machar alipanga njama za kuipinduwa serikali ya rais Kiir ndizo zilizosababisha  vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013.

Serikali ilivunjika 2016

Julai mwaka 2016, serikali ya muungano baina ya mahasimu hao wawili ilivunjika baada ya wanajeshi wao kupigana mjini Juba.

Juhudi za awali za kuunda serikali ya muungano hazikufaulu kutokana na tofauti baina ya Kiir na Machar kuhusu hasa muundo wa jeshi la kitaifa, idadi ya majimbo na usalama wa Riek Machar.

Rais Salva Kiir ametoa mwito kwa wakimbizi zaidi ya laki moja na tisini elfu wanaoishi kwenye makambi cchini ya ulizi wa umoja wa mataifa kurejea makwao. Machafuko ya Sudan Kusini yalisababisha vifo va watu laki tatu na mia nane elfu na zaidi ya milioni wengine kuyakimbia makaazi yao.

Pande zote mbili zimekuwa zikinyosheana kidole cha lawama. Kundi la Machar linalilaumu kundi la rais Kiir kwa kushindwa kuiongoza nchi.

Makubaliano hayo yamekuja  kufuatia shinikizo kutoka kwa Umoja wa Mataifa na Marekani la kutishia kuidhinisha vikwazo dhidi ya watu wa Sudan Kusini iwapo hakutoafikiwa makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ifikapo Jumamosi.

Tayari Marekani imepongeza taarifa za kuwepo na makubaliano baina ya viongozi hao wawili na kusema iko tayari kuunga mkono serikali mpya itakayounda.