Sadio Mane ashinda tuzo ya mchezaji bora Afrika- 2019 | Matukio ya Afrika | DW | 08.01.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Sadio Mane ashinda tuzo ya mchezaji bora Afrika- 2019

Mane raia wa Senegal, mwenye umri wa miaka 27 amewapiku Mohamed Salah kutoka Misri na Riyad Mahrez raia wa Algeria, na kushinda tuzo ya mchezaji bora Afrika mwaka 2019.

Mchezaji wa Liverpool, Sadio Mane ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa Afrika kwa mwaka 2019.

Mane raia wa Senegal, mwenye umri wa miaka 27 alikuwa akishindana na Mohamed Salah kutoka Misri na Riyad Mahrez raia wa Algeria.

Akizungumza baada ya ushindi huo katika sherehe zilizoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF na kufanyika Hurghada, Misri, Mane amesema amefurahi sana na anajivunia kushinda tuzo hiyo.

Tuzo ya mchezaji bora kijana imechukuliwa na Achraf Hakimi wa Morocco ambaye anaichezea Borussia Dortmund.

Asisat Oshoala wa Nigeria ameshinda kwa mara ya nne tuzo ya mchezaji bora wa kike wa Afrika.

Djamel Belmadi kutoka Algeria, ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka. Algeria imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka na Shirikisho la Soka la Misri limeshinda tuzo ya shirikisho bora la mwaka.