1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Saarland

Saarland, liliopo magharibi ya mbali mwa Ujerumani, ndiyo mmoja ya majimbo 16 ya shirikisho (Bundesländer). Mji wake mkuu ni Saarbrücken. Jimbo hilo ndiyo dogo zaidi mbali na majimbo ya miji - Berlin, Bremen na Hamburg.

Saarland ina eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 2,570 na wakaazi wake wanakadiriwa kuwa 1,012,000. Nyakati zilizopita jimbo hilo lilikuwa maarufu kwa uchimbaji wa makaa ya mawe, lakini hivi sasa sekta za magari, chuma na ufinyanzi zinatoa mchango muhimu.