1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rusesabagina awasili Marekani baada ya kuachiwa huru Rwanda

Hawa Bihoga
30 Machi 2023

Mkosoaji wa serikali ya Rwanda Paul Rusesabagina ambae juhudi zake za kuokoa watu wakati wa mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 zilichochea filamu ya Hollywood "Hotel Rwanda," amewasili Marekani

https://p.dw.com/p/4PU5l
Ruanda Paul Rusesabagina
Picha: Cyril Ndegeya/Xinhua/IMAGO

Rusesabagina amewasili nchini humo baada ya kuachiliwa kutoka gerezani huko Kigali. Mshauri wa masuala ya usalama nchini Marekani Jake Sullivan amethibitisha kuwasili kwa Rusesabagina, kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Rusesabagina aliachiliwa huru mwishoni mwa juma lililopita akuzuiliwa gerezani kwa zaidi ya siku 900, baada ya serikali ya Kigali kubadilisha kifungo chake cha miaka 25 kwa tuhuma za ugaidi, tuhuma ambazo wafuasi wake walizikanusha.

Rusesabagina awasili Qatar

Kuzuiliwa kwake kumeimulika Rwanda dhidi ya rekodi yake ya kukandamiza upinzani wa kisiasa na uhuru wa kujieleza chini ya Rais Paul Kagame.