Rosberg ana matumaini ya kutwaa ubingwa | Michezo | DW | 07.11.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Rosberg ana matumaini ya kutwaa ubingwa

Nico Rosberg wa mashindano ya magari ya Formula One amesema ana furaha kwa sababu angali na fursa ya kutwaa taji la ubingwa wa ulimwengu kwa kumpiku mwenzake wa timu ya Mercedes Lewis Hamilton.

Huku zikiwa zimesalia mbio mbili pekee msimu ukikamilika, Rorberg yuko nyuma y Hamilton na tofauti ya points 24 kati yao na huku kukiwa na points mara mbili za kushindaniwa katika mbio za mwisho za msimu za Abu Dhabi, Rosberg angali na matumaini ya kumpiku Muingereza Hamilton katika ubingwa wa ulimwengu.

Rosberg aliyasema hayo nchini Brazil wakati akijiandaa kwa mashindano ya kesho Jumapili katika uwanja wa mbio za magari wa Interlagos.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu