Ronaldo aambukizwa virusi vya corona | Michezo | DW | 13.10.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ronaldo aambukizwa virusi vya corona

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno na mshambuliaji wa Juventus Turin Cristiano Ronaldo amekutikana na virusi vya Corona. Taarifa hiyo imethibitishwa na shirikisho la soka nchini Ureno FPF

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno na mshambuliaji wa Juventus Turin Cristiano Ronaldo amekutikana na virusi vya Corona. Taarifa hiyo imethibitishwa na shirikisho la soka nchini Ureno FPF. Taarifa hiyo imeeleza kuwa staa huyo hakuonyesha dalili zozote za ugonjwa wa COVID-19 na kuwa ameamua kujitenga kwa mujibu wa kanuni za afya. Hali hiyo ina maana kuwa ataikosa mechi ya ligi ya mataifa ya Ulaya dhidi ya Sweden. Ronaldo mwenye umri wa miaka 35 anatarajiwa pia kuzikosa mechi kadhaa za klabu yake ya Juventus inayoshiriki ligi ya Italia ya Serie A.