1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya Mali yajadiliwa na Baraza la Usalama.

Sudi Mnette
9 Oktoba 2020

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Mali amewataka raia wa taifa hilo la Afrika Magharibi kuachana na harakati za mara kwa mara za kulirejesha taifa hilo katika machafuko yanayotokana na mapinduzi ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/3jf11
Mali Militär
Picha: AFP

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Mali, Mahmat Saleh Annadif amewataka raia wa taifa hilo la Afrika Magharibi ambao wamesishi katika matukio mfulilozo ya mapinduzi ya kijeshi kutumia miezi 18 ya kipindi cha mpito kuliondoa taifa hilo katika hali ya kujirejea ya mapinduzi, ambayo yamelisababisha taifa hilo kusalia katika mgogoro.

Mahmat Saleh Annadif  amelieleza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba mafanikia katika kipindi cha mpito yapo katika mkondo mzuri na kwamba vikwazo vitasalia kwa raia wa Mali wenyewe. Taarifa ya Annadif ni ya kwanza kuwasilishwa kwa baraza hilo tangu kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 18, ambayo yalimuondoa madarakani Rais Ibrahim Baoubakar Keita.

Balozi wa Ufarasa ataka kuimarishwa demokrasia ya Mali

Alisema mali haina serikali kwa takribani miezi minne sasa, na kuondolewa vikwazo kwa taifa hilo kutafanikisha uwepo wa serikali itakayoongoza kisheria. Balozi wa Ufaransa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  Nicolas De Riviere aliihamasisha mamlaka mpya ya Mali kujenga misingi ya taasisi imara ya kidemokrasia, kuanzisha upya utekelezaji wa makubaliano ya amani ya 2015 na kurejesha amani katika eneo la katikati ya taifa hilo.

Kwa upande wake Balozi wa Mali katika baraza hilo, Issa Konfourou aliliambia baraza kwamba raia na wanajeshi ambao walikamatwa na kuwekwa kizuizini, kwa kuunganishwa na mapinduzi ya Agosti 18 wameachiwa Jumatatu iliyopita. 

Mateka mfaransa wa umri wa miaka 75 aachiwa huru

Malische Geiseln befreit
Mfarasa aliyechukuliwa mateka kwa miaka 4, Sophie PetroninPicha: AP Photo/picture-alliance

Hatua hiyo inakwenda sambaba na serikali ya Mali kuwaachia huru wapigaji zaidi ya 200 wenye itakaidi kali jambo lililojibiwa pia kwa kuachiwa huru kwa mfanyakazi wa huduma ya kiutu wa Ufaransa, Sophie Petronin mwenye umri wa miaka 75 pamoja na mateka wengine wawili Waitaliano. Sophie alitekwa 2016.

Katika ukurasa wake wa Twetter, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amemkabiribisha nyumbani Petrinin, ambae anatajwa kuwa mfarasa wa mwisho kukamatwa mateka dunania katika kipindi hiki. Mpango huo pia wa kubadilishana wafungwa umemnusuru mgombea urais wa Mali kwa mara tatu, Soumaila Cisse ambae nae alituwa katika uwanja wa ndege wa Bamako baada ya kuachiwa huru.

Soma zaidi:Rais wa mpito aapishwa Mali baada ya mapinduzi

Mali imekuwa katika machafuko tangu  ghasia za 2012, ambazo zilisababisha uasi wa kumuondoa madarakani rais, lilizuka uombwe la uongozi, ambalo lilisababisha pia uasi wa makundi ya wenye itikadi kali ambapo Ufaransa ikiangia 2013 katika taifa hilo kuongoza vita vya kuyaondoa makundi hayo madarakani.

Mwandishi: Sudi Mnette APE