Rio kuweka usalama wakati wa Olimpiki | Michezo | DW | 31.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Rio kuweka usalama wakati wa Olimpiki

Operesheni ya usalama inayopangwa kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro mwaka ujao ndio itakayokuwa operesheni kubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo

Waziri wa usalama na matamasha makubwa Andrei Rodrigues amesema muhimu katika operesheni hiyo ni kuletwa pamoja vitengo tofauti, na karibu maafisa 85,000 watahusishwa.

Michezo hiyo itaandaliwa katika maeneo 33 ya mjini Rio na viwanja vitano vya kandanda kote nchini humo, wakati Mwenge wa Olimpiki utaifika katika miji 250 ya Brazil.

Mwakilishi wa Shirika la ujasusi la Brazil Saulo Moura anasema kituo cha ujasusi kitakachoshughulikia tu ugaidi kitawekwa mjini Rio karibu na michezo hiyo. Alisema "hakuna dalili kuwa tunakabiliwa na kitisho chochote cha ugaidi. Hata hivyo, narudia tena, kama ilivyotokea katika michezo ya nyuma, Brazil itakuwa mwenyeji wa tamasha litakaloyavutia makundi ya itikadi kali. Ni kwa sababu hiyo ambapo tunaichunguza hali, huku kitengo maalum kikishughulikia ugaidi ndani ya shirika la ujasusi".

Shirika la ujasusi pia litashirikiana na mataifa yatakayoshiriki tamasha hilo katika kubadilishana habari zinazolenga kuzuia matukio ya kigaidi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters/AP/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef