Ribery aumia tena wiki moja baada ya kurejea | Michezo | DW | 11.12.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Ribery aumia tena wiki moja baada ya kurejea

Aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Franck Ribery atakosa michuano mitatu ya Bayern ya mwisho wa mwaka wa 2015 baada ya kuumia paja.

Ribery alirudi kikosini wiki moja iliyopita baada ya kuwa mkekani kwa muda wa miezi tisa. Aliuanza mchuano wa Champions League Jumatano walioishinda Dinamo Zagreb mabao mawili kwa sifuri lakini akalazimika kuondoka uwanjani katika kipindi cha mapumziko kutokana na tatizo la msuli katika paja lake la kulia.

Hata hivyo watalaamu wanasema tatizo hilo sio kubwa sana, na ni hatua ya tahadhari tu iliyochukuliwa kumpumzisha. Beki wa Bayern, Mmorocco Mehdi Benatia pia atakuwa nje katika kipindi kilichosalia cha 2015 kutokana na maumivu kama hayo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Iddi Sessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com