Ribery akaribia kurudi tena uwanjani | Michezo | DW | 12.10.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ribery akaribia kurudi tena uwanjani

Mchezaji nyota wa kiungo wa Bayern Munich, Mfaransa Frank Ribery anakaribia kurudi tena uwanjani, kufuatia kasi ya mazoezi ya kiungo kwa msada wa mashine ya kisasa

Mashine hiyo ilivumbuliwa na Wakala wa safari za anga wa Marekani – NASA na ambao hutumiwa kuwapa mazoezi wanaanga. Ribery amekua nje ya uwanja kwa miezi 7 sasa, tokea alipoumia katika mchezo wa ubingwa wa ligi za vilabu vya Ulaya –Champions league mwezi Machi.

Taarifa zinasema sasa ameanza kupata nafuu ya haraka ya majeraha ya mguu wake wa kulia. Hadi sasa Ribery mwenye umri wa miaka 32 ameshakosa michuano 28 ya miamba ya ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga- Bayern Munich , ikiwa ni pamoja na ule wa Jumapili iliopita ambapo waliitandika Borussia Dortmund mabao 5-1 na sasa wako kileleni wakiwa na pointi 4 zaidi ya Dortmund inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo .

Kikosi cha kocha Pep guardiola pia kimekuwa uwanjani bila ya Mholanzi wingi wa kulia Arjen Robben ambaye pia amejeruhiwa. Guardiola anatarajia Robben ataweza kurudi uwanjani kwa pambano la ligi Oktoba 17 dhidi ya Werder Bremen . Nafasi za Ribery na Robben zimejazwa na kiungo Kingsley Coman –mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa chini ya miaka 21 na wingi wa Brazil Douglas Costa.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman, afp,dpa,rtr
Mhariri:Yusuf Saumu