1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Zelenskiy autembelea mkoa wa kusini kuwaona makamanda

15 Agosti 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ameutembelea mkoa wa kusini mashariki wa Zaporizhzhia na kukutana na wapiganaji waliokuwa mstari mbele vitani

https://p.dw.com/p/4VCke
BG | Wolodymyr Selenskyj
Picha: Ukrainian Presidential Press Service/Handout/REUTERS

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya kiongozi huyo imesema Zelensky amepokea ripoti kutoka kwa makamanda wa jeshi kuhusu mwelekeo wa mapambano kwenye maeeno kadhaa ya uwanja wa vita.

Soma pia: Zelensky ameapa kulipiza kisasi baada ya kuuwawa watu wanne karibu na Kherson

Pia amejadiliana na maafisa wa jeshi juu ya changamoto zinazowabalii katika wakati Urusi imezidisha hujuma kote nchini humo wakiilenga miji kwa makombora  na kuharibu miundombinu.

Jeshi la Ukraine limesema hii leo Urusi imevurumisha makombora ya 28 ya masafa yaliyowajeruhwa watu 19 kwenye mji wa magharibi wa Lviv. Afisa mmoja wa serikali ya Ukraine amesema mashambulizi hayo yanalenga kuwaua watu na kuwavunja moyo raia wa taifa hilo.