1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Syria aalikwa katika mikutano muhimu Dubai

16 Mei 2023

Kiongozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, amemwalika Rais wa Syria Bashar al-Assad kuhudhuria mkutano ujao wa Mabadiliko ya Tabianchi wa COP28 utakaofanyika Novemba 30 huko Dubai.

https://p.dw.com/p/4RPGm
Syrien Präsident Bashar al-Assad
Picha: Joseph Eid/AFP/Getty Images

Kufuatia kurejeshwa tena kwa Syria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Assad anatarajiwa pia kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya hiyo unaotarajiwa kufanyika mjini Jeddah siku ya Ijumaa.

Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock akiwa ziarani nchini Saudia, ametahadharisha juu ya kurejesha uhusiano na rais wa Syria, Bashar al-Assad bila ya kumpa masharti.

Baada ya mkutano hapo jana na mwenzake wa Saudia Faisal bin Farhan kwenye mji wa mwambao wa bahari ya Shamu wa Jeddah , Baerbock amesisitiza kuwa Assad hapaswi kutuzwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.