Rais wa Brazil hatimaye ajitokeza | Matukio ya Kisiasa | DW | 22.06.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Rais wa Brazil hatimaye ajitokeza

Rais wa Brazil Dilma Rousseff amemaliza ukimya aliokuwa nao juu ya maandamano makubwa ya ghasia, akisema kuwa maandamano ya amani ni sehemu ya demokrasia imara lakini ghasia haziwezi kuvumilika.

Brazilian President Dilma Rousseff delivers a speech during a ceremony at Planalto Palace in Brasilia, on June 18, 2013. Rousseff said Tuesday that the voices of the hundreds of thousands of youths protesting across Brazil over the huge cost of hosting sporting events like the World Cup must be heard. AFP PHOTO / Evaristo SA (Photo credit should read EVARISTO SA/AFP/Getty Images)

Rais wa Brazil Dilma Rousseff

Ameahidi kuimarisha huduma za umma na kufanya mazungumzo na viongozi wa maandamano.

Lakini bado haifahamiki hasa nani anaweza kuwakilisha makundi makubwa ambayo hayana uongozi ya waandamanaji wanaoingia mitaani, wakitoa hasira zao dhidi ya huduma mbovu za umma licha ya mzigo mkubwa wa kodi unaowakabili.

RIO DE JANEIRO, BRAZIL - JUNE 20: Protestors display banners during the FIFA Confederations Cup Brazil 2013 Group B match between Spain and Tahiti at the Maracana Stadium on June 20, 2013 in Rio de Janeiro, Brazil. (Photo by Ronald Martinez/Getty Images)

Waandamanaji wakionesha bango

"Nitakutana na viongozi wa maandamano ya amani, nataka taasisi ambazo ziko wazi zaidi , zinaopinga matendo mabaya," Rousseff amesema akimaanisha hisia za rushwa katika siasa za Brazil, hali ambayo inajitokeza kama lengo la maandamano hayo. "Raia wake na sio uwezo wa kiuchumi ndio unapaswa kuwa mbele."

Waandamanaji wanataka huduma bora

Licha ya kuwa hakutoa maelezo zaidi , Rousseff amesema kuwa serikali yake itatengeneza mpango maalum wa kitaifa kwa ajili ya usafiri wa umma katika miji, kupanda kwa nauli za mabasi na treni za mijini lilikuwa ni lalamiko la msingi la waandamanaji.

RIO DE JANEIRO, BRAZIL - JUNE 20: Protestors display banners during the FIFA Confederations Cup Brazil 2013 Group B match between Spain and Tahiti at the Maracana Stadium on June 20, 2013 in Rio de Janeiro, Brazil. (Photo by Alexandre Loureiro/Getty Images)

Maandamano yakiendelea mjini Rio

Pia amerudia uungaji wake mkono wa mpango ulioko katika bunge la nchi hiyo kuwekeza mapato yote ya mafuta katika elimu na ahadi aliyoitoa hapo kabla ya kuwaleta madaktari kutoka nje katika maeneo ambayo yanakosa waganga.

Kiongozi huyo ambaye ni muasi wa zamani wa kundi la kikomunist ambaye amepambana dhidi ya utawala wa kijeshi wa Brazil mwaka 1964 hadi 1985 na alifungwa kwa muda wa miaka mitatu na kuteswa na utawala huo wa kijeshi, ameelezea kuhusu alivyojitolea muhanga hapo kabla kulifanya taifa hilo kuwa huru kutokana na utawala wa kidikteta.

A demonstrator holds a sign that reads, Brazil, a country of theft, during an anti-government protest in Porto Alegre, southern Brazil, June 20, 2013. Tens of thousands of demonstrators marched through the streets of Brazil's biggest cities on Thursday in a growing protest that is tapping into widespread anger at poor public services, police violence and government corruption. REUTERS/Gustavo Vara (BRAZIL - Tags: CIVIL UNREST POLITICS BUSINESS EMPLOYMENT SPORT SOCCER)

Mwandamanaji akibeba bango linalosema "Brazil nchi ya wezi".

"Kizazi changu kilipambana mno ili sauti katika mitaa ziweze kusikika," Rousseff amesema . "Wengi walishtakiwa, waliteswa na wengi wameuwawa kwa ajili hiyo. Sauti za mitaani ni lazima zisikike na kuheshimiwa na zinaweza kufikiriwa vibaya kwamba ni kelele na ghasia za baadhi ya watu wanaopenda kufanya ghasia.

Akosolewa

Amekosolewa kwa kiasi kikubwa kwa kutoonekana na kujali huku maandamano yakifanyika na kushindwa kuhusika na jamii ambayo inadai serikali yake iwasikilize.

Edvaldo Chaves , mwenye umri wa miaka 61 mlinzi wa nyumbani katika kitongoji kinachokaliwa na watu wenye uwezo kiasi cha Flamengo mjini Rio, amesema ameiona hotuba aliyotoa Rousseff siku ya Ijumaa kuwa inaridhisha.

"Nafikiri alikuwa mtulivu na alifanya kazi nzuri. Pamoja na kwamba , kwasababu alikuwa mpiganaji na aliishi uhamishoni , anazungumzia masuala ya waandamanaji kwa uhakika zaidi," Chaves amesema. "Nafikiri mambo yatatulia sasa. Huenda tutaendelea kuwaona watu mitaani lakini huenda itakuwa ni idadi ndogo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / ape

Mhariri: Bruce Amani

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com