1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Confederations Cup; Maandamano yatia doa

22 Juni 2013

Michuano ya kombe la mabara, Confederations Cup, yaingia doa, waandamanaji wadai serikali ya Brazil inapaswa kuwekeza zaidi katika elimu, afya na miundo mbinu badala ya ujenzi wa viwanja vya soka.

https://p.dw.com/p/18u6P
Demonstrators protest against the Confederation's Cup and the government of Brazil's President Dilma Rousseff outside the national congress in Brasilia June 17, 2013. Tens of thousands of demonstrators marched through the streets of Brazil's biggest cities on Monday in a growing protest that is tapping into widespread anger at poor public services, police violence and government corruption. Protesters are using the Confederation's Cup as a counterpoint to amplify their concerns. REUTERS/Ueslei Marcelino (BRAZIL - Tags: POLITICS CIVIL UNREST SPORT SOCCER TPX IMAGES OF THE DAY) TEMPLATE OUT
Maandamano wakati wa kombe la Confed nchini BrazilPicha: Reuters

Brazil na Italia zinapambana kuwaepuka mabingwa wa dunia Uhispania katika nusu fainali.

Matumaini ya Japan na Mexico katika Confederations Cup yafikia ukingoni , na katika tennis uwanja utayari kwa mpambano wa kuwania taji la Wimbledon , kwa hayo na mengineyo huyu hapa Sekione Kitojo.

Rais wa Brazil Dilma Rousseff ameitisha kikao cha dharura cha baraza la mawaziri jana Ijumaa(20.06.2013), siku moja baada ya mtu mmoja kuuwawa katika maandamano na watu wanaokadiriwa kufikia milioni1 na 225,000 kuingia mitaani nchi nzima wakidai huduma bora za umma.

June 18, 2013 - Sao Paulo - A man runs through the burning streets as demonstrators take part in a protest organized by the Pase Libre Movement. Brazil's government says it will deploy a national security force to five major cities after a wave of protests which has seen almost a quarter of a million people demand better public services. The national force will be sent to Rio de Janeiro, Belo Horizonte, Salvador, Fortaleza and the capital, Brasilia. All of the cities are hosting games in Fifa's Confederations Cup
Mandamano nchini BrazilPicha: picture alliance / ZUMA Press

Maandamano hayo makubwa , ambayo katika baadhi ya nyakati yalifikia kuwa ni mapambano ya kutumia nguvu, yanafanyika wakati Brazil ambayo watu wake wanafahamika kuwa na wazimu wa soka ni mwenyeji wa mashindano makubwa ya kombe la mabara, ambapo timu za mataifa kutoka sehemu mbali mbali za dunia zinashiriki mashindano hayo, ikiwa ni majaribio ya fainali za kombe la dunia mwakani nchini humo.

Wabrazil wakasirika

Wabrazil wengi wamekasirishwa na matayarisho ya gharama kwa ajili ya michezo hiyo ya kombe la dunia na michezo ya Olimpiki ya majira ya joto mwaka 2016.

Waandamanaji kadha wameendelea kubaki nje ya viwanja vinavyofanyika mashindano hayo , na maandamano makubwa kabisa yanapangwa kufanyika Juni 30 katika uwanja maarufu wa Maracana mjini Rio de Janeiro katika siku ya fainali ya kombe la Confederations.

Wakati huo huo vigogo wa soka duniani Brazil pamoja na Italia watapambana kuwaepuka mabingwa wa dunia Hispania wakati watakapokutana katika mchezo wa mwisho wa duru ya makundi katika kombe la Cofederations mjini Salvador leo jioni(22.06.2013).

epa03752032 Neymar (L) of Brazil and Marcelo (R)react after scoring against Mexico during the match between Brazil and Mexico at the FIFA Confederations Cup 2013 in Fortaleza, Brazil, 19 June 2013. EPA/ROBERT GHEMENT +++(c) dpa - Bildfunk+++
Wachezaji wa Brazil wakishangiria baoPicha: picture-alliance/dpa

Mchezo huo wa kundi A unazikutanisha timu hizo mbili zenye mafanikio makubwa katika historia ya kombe la dunia, wakati wenyeji Brazil wanashikilia rekodi ya kulinyakua kombe la dunia mara tano wakati Italia imelinyakua mara nne.

Timu zote zina points sita baada ya ushindi mara mbili, lakini timu itakayomaliza ikiwa ya kwanza katika kundi hilo huenda ikaiepuka Uhispania ambayo ina nafasi kubwa ya kushika nafasi ya kwanza katika kundi B.

Mratibu wa masuala ya ufundi katika timu ya Brazil Carlos Alberto Pereira amesema kocha Luiz Felipe Scolari huenda asiwatumie wachezaji ambao hawako fit ili kuweza kuwapata kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali.

Palmeiras head coach Luiz Felipe Scolari talks to his players during their Copa Sudamericana 2010 football semifinals match against Goias, at Serra Dourada stadium in Goiania, Brazil on November 17, 2010. AFP PHOTO/Evaristo SA (Photo credit should read EVARISTO SA/AFP/Getty Images)
Kocha mkuu wa Brazil Luiz Felipe ScolariPicha: EVARISTO SA/AFP/Getty Images

Baadhi ya wachezaji katika kikosi cha Scolari ni majeruhi , hususan baada ya mchezaji wa kati Paulihno kupata maumivu katika kifundo cha mguu, na mlinzi wa kati David Luiz kupata maumivu ya pua, katika mchezo dhidi ya Mexico.

Nyota wa Italia Andrea Pirlo atakuwa nje ya uwanja leo kwa kuwa ana maumivu ya paja. Pamoja na Pirlo mchezaji Daniele De Rossi hatakuwamo katika kikosi cha kocha Cesare Prandelli kutokana kupata kadi ya pili ya njano. Brazil inahitaji sare kushika nafasi ya kwanza na kuiepuka Uhispania katika nusu fainali.

RIO DE JANEIRO, BRAZIL - JUNE 20: David Villa of Spain celebrates scoring his team's fourth goal during the FIFA Confederations Cup Brazil 2013 Group B match between Spain and Tahiti at the Maracana Stadium on June 20, 2013 in Rio de Janeiro, Brazil. (Photo by Alexandre Loureiro/Getty Images)
Mchezaji wa Uhispania David VillaPicha: Getty Images

Matumaini yaota mbawa

Japan na Mexico ziliingia katika mashindano haya kwa matumaini makubwa ya kusonga mbele, lakini matumaini hayo yameopta mbawa chini ya wiki moja baada ya michuano hiyo kuanza baada ya timu hizo kushindwa kupata ushindi katika michezo yao dhidi ya wenyeji Brazil ama Italia.

Timu hizo hata hivyo zinakutana katika mchezo wa kutimiza wajibu leo mjini Belo Horizonte.

Tennis

Na mashabiki wa mchezo wa tennis watapata nafasi ya kushuhudia nyota wa mchezo huo wakichuana katika kuwania taji maarufu la mchezo huo la Wimbledon kuanzia kesho Jumapili.

Bingwa mara saba wa taji hilo Roger Federer huenda akapambana na hasimu wake mkubwa Rafael Nadal katika robo fainali ya michuano hiyo ya Grand Slam ya Wimbledon.

Federer na Nadal wamepangwa katika kundi moja na Andy Murray pia yumo katika kundi hilo na anaweza kukutana na Nadal ama Federer katika nusu fainali.

Mwandishi: Sekione Kitojo / ape / dpae / rtre

Mhariri:Abdul-Rahman Mohammed