1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Faye aagiza mpango kazi wa kuimarisha uchumi

Mohammed Khelef
10 Aprili 2024

Rais Bassirou Diomaye Faye wa Senegal amemuagiza waziri wake mkuu kuwasilisha mpango kazi wa haraka wa kuimarisha uchumi na sekta ya fedha.

https://p.dw.com/p/4ebDR
Bassirou Diomaye
Rais mpya wa Senegal Bassirou Diomaye Faye Picha: John Wessels/AFP

Taarifa iliyotolewa jana na ofisi ya kiongozi mwenye umri wa miaka 44 aliyeingia madarakani kwa ahadi ya kuleta mageuzi makubwa na ya haraka, imesema Faye amemtaka Waziri Mkuu Ousmane Sonko kufanya mapitio makubwa ya programu na mipango na kuwasilisha ripoti ya hali ya kifedha ya nchi, mashirika ya kimataifa na ubia baina ya serikali na sekta binafsi.

Hili ni agizo la kwanza la rais huyo baada ya kikao cha kwanza cha baraza la mawaziri.

Waziri Mkuu wa Senegal atangaza serikali yake mpya

Sonko, ambaye ni mshirika wa karibu wa Faye, alisema wakati wa kulitangaza baraza lake la mawaziri siku ya Ijumaa kwamba vipaumbele vya serikali yake vitajumuisha ajira kwa vijana, kupunguza gharama za maisha na kulinda haki za binaadamu.

Kampuni na wawekezaji wa kigeni wanatiwa wasiwasi na kile wanachosema ni misimamo mikali ya mageuzi ya viongozi hao wapya wa Senegal.