Rais Kibaki autengua uteuzi wake,Kenya
22 Februari 2011Matangazo
Uteuzi huo ulifanyika mwezi uliopita na ulizua mitazamo na hisia tofauti katika serikali ya Kenya ya muungano wa Kitaifa.Rais Kibaki aliwateua Jaji Mkuu mpya,Mwanasheria Mkuu,Mwendesha mashtaka pamoja na Msimamizi wa Bajeti.Hata hivyo utata ulizuka baada ya Waziri Mkuu raila Odinga kusema kuwa hakuhusishwa katika shughuli hiyo,jambo lililosababisha mvutano.
Rais Kibaki alisisitiza kuwa kamwe hakuikiuka katiba na aliyatimiza majukumu yake kama anavyoruhusiwa.Hata hivyo itakumbukwa kuwa Spika wa Bunge la Kenya,Kenneth Marende,alisema kuwa uteuzi huo uliikiuka katiba.Mahakama Kuu iliyoko mjini Nairobi nayo pia iliuunga mkono mtazamo huo.