1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Faye amteua Sonko kama Waziri Mkuu wa Senegal

3 Aprili 2024

Rais mpya wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, amemteua mwanasiasa mkuu wa upinzani na muungaji mkono wake mkubwa Ousmane Sonko kama waziri mkuu wa nchi hiyo, katika uteuzi wake wa kwanza kama rais.

https://p.dw.com/p/4eNdL
Senegal Dakar |  Ousmane Sonko
Aliyekuwa kiongozi wa upinzani Senegal Ousmane SonkoPicha: Annika Hammerschlag/AA/picture alliance

Rais mpya wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, amemteua mwanasiasa mkuu wa upinzani na muungaji mkono wake mkubwa Ousmane Sonko kama waziri mkuuwa nchi hiyo, katika uteuzi wake wa kwanza kama rais.

Akizungumza mara tu baada ya uteuzi wake, Sonko amesema atawasilisha orodha ya mawaziri anaowapendekeza kwa Rais Faye kwa ajili ya idhini yake.

Sonko na Faye walifanya kampeni kwa pamoja chini ya kauli mbiu "Diomaye ni Sonko" na Sonko akawataka wafuasi wake wampigie kura Faye ambaye hatimaye alishinda kwa asilimia 54 katika raundi ya kwanza.

Soma: Faye analenga kuibadilisha Senegal kiuchumi kwa kutumia gesi na mafuta

Sonko alikuwa mpinzani mkubwa wa rais wa zamani Macky Sall na ana umaarufu mkubwa miongoni mwa vijana wa nchi hiyo ila alikuwa na marufuku ya kushiriki uchaguzi huo kutokana na kesi inayomkabili mahakamani.