1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Sonko ateuliwa kuwa waziri mkuu wa Senegal

Tatu Karema
3 Aprili 2024

Rais mpya wa Senegal Bassirou Diomaye Faye amemteuwa kiongozi maarufu wa upinzani Ousmane Sonko, kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo, saa chache baada ya kuapishwa kwake jana kuwa rais wa tano wa Senegal

https://p.dw.com/p/4eMuT
Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko akihutubia wakati wa mkutano wa hadhara wa chama chake mjini Dakar mnamo Juni 8, 2022
Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane SonkoPicha: Seyllou/AFP

Oumar Samba Ba, katibu mkuu katika ofisi ya Rais, alitangaza uteuzi huo wa Sonko kupitia agizo la Rais lililopeperushwa kwenye kituo cha televisheni cha umma RTS.

Sonko asema atawasilisha orodha ya mawaziri kwa Rais

Akizungumza baada ya kuteuliwa kwake, Sonko alisema kuwa atawasilisha kwa Rais orodha kamili ya mapendekezo ya uteuzi wa mawaziri ili kuidhinisha.

Sonko ameongeza kuwa hatamuacha Rais kukabiliana na jukumu hilo zito peke yake.

Sonko alizuiliwa kugombea katika uchaguzi wa urais

Sonko, mpinzani wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Macky Sall, ni maarufu miongoni mwa vijana nchini humo lakini alizuiliwa kugombea katika uchaguzi wa urais wa Machi 24 kutokana na mashtaka ya kuharibia sifa.

Hata hivyo alikanusha madai hayo.