Rais Bashir amemfuta kazi waziri wa mambo ya nchi za nje | Matukio ya Afrika | DW | 20.04.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Rais Bashir amemfuta kazi waziri wa mambo ya nchi za nje

Shirika la habari la serikali SUNA limeripoti kwamba waziri Ibrahim Ghandour alitimuliwa baada ya kusema wanadiplomasia wa Sudan katika mataifa ya kigeni hawajalipwa mishahara kwa miezi kadhaa

Rais wa Sudan Omar Hassan al Bashir amemfuta kazi waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa nchi hiyo Ibrahim Ghandour. Shirika la habari la serikali SUNA limeripoti kwamba waziri huyo alitimuliwa baada ya kusema wanadiplomasia wa Sudan katika mataifa ya kigeni hawajalipwa mishahara kwa miezi kadhaa.

Katika hotuba yake kwa wabunge hapo jana Ghandour, aliyeongoza mazungumzo ya kuondolewa vikwazo vya muongo mmoja vilivyowekwa na Marekani mnamo Oktoba mwaka uliopita, alisema wizara yake pia ilikuwa imeshindwa kulipa kodi kwa balozi kadhaa za Sudan kwa sababu ya mapungufu ya fedha serikalini.

Sudan imekabiliwa na matatizo ya fedha huku ikikabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni ambao umesababisha uchumi wa taifa hilo la Afrika Mashariki kuendelea kudorora.

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com