Wafungwa wa kisiada Sudan kuachiwa
11 Aprili 2018Matangazo
Rais Omar al-Bashir wa Sudan ameamrisha kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa wiki kadhaa baada ya kamatakamata dhidi ya waandamanaji waliokuwa wanaipinga serikali.
Maafisa wa usalama waliwakamata mamia ya viongozi wa upinzani, wanaharakati na waandamanaji, mwezi Januari katika jaribio la kusitisha maandamano kuhusiana na kuongezeka kwa bei za chakula, ikiwemo mkate.
Shirika la habari la serikali la SUNA limetangaza kwamba Rais Bashir ametoa "amri ya kuachiwa kwa wafungwa wote wa kisiasa waliozuiliwa kote nchini."
Shirika hilo la habari halikueleza ni wafungwa wangapi watakaoachiwa na halikusema pia iwapo wafungwa waliokuwa wanazuiwa kabla kamatakamata hiyo wataachiwa pia au la.