SiasaBangladesh
Raia wa Bangladesh wapiga kura tangu vuguvugu la 2024
12 Februari 2026
Matangazo
Usalama umeimarishwa kote nchini humo wakati uchaguzi huo pamoja na kura ya maoni kuhusu mageuzi ya katiba vikiendelea, ambapo vikosi vya usalama zaidi ya 900,000 vikiwa vimesambazwa.
Mamlaka zimesema zinataka kuhakikisha kunakuwepo na usalama katika kila hatua katikati ya hali tete ya kisiasa chini Bangladesh.
Mkuu wa Tume ya Uchaguzi Nasir Uddin amezihimiza pande zinazohasimiana na wapiga kura kulitekeleza zoezi hilo kwa utulivu na kukubali matokeo, licha ya tofauti za maoni.
Mshauri wa Mambo ya Ndani Jahangair Alam Chowdhury ameonya hatua kali zinaweza kuchukuliwa dhidi ya jaribio lolote la kuvuruga uchaguzi.