1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PSV Eindhoven walinusa taji la Eridivise

4 Machi 2024

Ni mwaka mmoja sasa tangu PSV Eindhoven ya Uholanzi ishindwe katika ligi ya nchini humo Eridivise na sasa wanaonekana kuwa njiani kulibeba taji kwa mara ya kwanza tangu 2018.

https://p.dw.com/p/4d9JR
Niederlande Eindhoven | Trainer PSV Eindhoven | Peter Bosz
Kocha wa PSV Eindhoven Peter BoszPicha: Bart Stoutjesdijk/ANP/picture alliance

Hapo Jumapili walikuwa nyuma katika mechi yao dhidi ya mabingwa watetezi Feyenoord ila walipambana na hatimaye kupata sare ya 2-2.

Kwa sasa wana uongozi wa pointi kumi kileleni wakiwa wameshinda mechi 21 na kutoka sare tatu katika mechi 24. Ni mechi 10 tu zilizosalia msimu kufikia mwisho.

Vyanzo: DPA/AP/Reuters