PORTMAO : Wazazi watuhumiwa kutoweka kwa mtoto wao | Habari za Ulimwengu | DW | 08.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PORTMAO : Wazazi watuhumiwa kutoweka kwa mtoto wao

Mama na baba wa msichana mdogo wa Uingereza Madeleine McCann ambaye alitoweka akiwa kwenye mapumziko na wazazi wake katika hoteli nchini Ureno wote wawili wametangazwa rasmi kuwa watuhumiwa kwenye tukio hilo.

Wazazi hao Kate na Gerry McCann wamehojiwa na polisi ya Ureno na wakili wao Carlos Pinto de Abreu amesema kwamba wazazi hao ambao wote ni madaktari sasa wako chini ya tuhuma na kwamba hakuna masharti ya dhamana yaliotolewa dhidi yao na wala hawakufunguliwa mashtaka.

Kutajwa wazazi hao kuwa watuhumiwa kumekuja baada ya polisi nchini Ureno kupokea sehemu ya matokeo ya uchunguzi wa maabara juu ya alama za damu zinazodaiwa kugunduliwa kwenye chumba ambapo msichana huyo wa miaka minne alikuwa amelala.

Kate alitoweka hapo tarehe 3 mwezi wa Mei na uchunguzi unaendelea.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com