PORT HARCOURT:Wapiganaji wavamia jela Port Harcourt | Habari za Ulimwengu | DW | 29.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PORT HARCOURT:Wapiganaji wavamia jela Port Harcourt

Kundi kuu la wapiganaji nchini Nigeria katika eneo la kusini lililo na mafuta mengi linakiri kuwa limeshambulia jela moja na kumwachia huru mmoja wa kiongozi wao aliyekuwa kizuizuini.

Kulingana na maafisa katika sekta ya mafuta mjini Port Harcourt tukio hilo lilitokea na kusababisha mpita njia mmoja kupoteza maisha yake pale wapiganaji hao walipofyatua baruti katika eneo hilo.Kwa mujibu wa kamishna wa polisi wa jimbo la Rivers Felix Ugbaudu hakuna maafisa wowote wa polisi waliojeruhiwa ila raia wa kawaida wachache pekee.

Kundi hilo lijulikanalo kama Movement for the Emancipation of the Niger Delta linasema kuwa jeshi lilipeleka wanajeshi wake waliojihami ili kupambana na wapiganaji wake 50 waliomnasua kiongozi wao na kumrejesha katika eneo lililo na mafuta mengi.Kulingana na kundi hilo wapiganaji wake walijihami kwa bunduki na guruneti wakati wa mapigano hayo yaliyodumu kwa saa moja.Hakuna mpiganaji yoyote wa kundi hilo aliyejeruhiwa au kuuawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com