Polisi wavamia vyombo vya habari Zambia | Matukio ya Afrika | DW | 16.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Polisi wavamia vyombo vya habari Zambia

Polisi wamevamia nyumba ya mhariri mkuu anayeikosoa serikali, lakini walishindwa kumkamata  kwa sababu alikuwa safarini nje ya nchi.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kwamba badala yake polisi walimkamata mke wa Fred M'membe, mhariri mkuu wa gazeti la The Post, ambalo lilifungwa mwezi Juni. Watu walioshuhudia wamesema polisi walitumia nguvu kumkamata  mke wa M'membe, Mutinta, na kwamba mwandishi habari Joan Chorwa alizuiwa kutoka katika nyumba hiyo wakati nyumba hiyo ilipovamiwa  jana. Polisi wengine zaidi  waliwasili  katika  nyumba hiyo leo. Uvamizi huo unafuatia hatua za M'membe kuweka pingamizi mahakamani dhidi ya kutaifishwa kwa mali za gazeti hilo la The Post, ambalo lilifungwa kwa misingi kwamba  lilikuwa na deni la  zaidi  ya dola milioni 4 katika malipo ya kodi. Gazeti hilo halijafanya kazi tangu Novemba 2 mwaka jana, wakati  lilipotakiwa kufilisiwa.