Polisi na vikosi vya kuzima moto vyakabiliwa na tatizo la mshahara Marekani | Masuala ya Jamii | DW | 03.08.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Polisi na vikosi vya kuzima moto vyakabiliwa na tatizo la mshahara Marekani

Kuanzia New York hadi California polisi na vikosi vya kuzima moto vyakabiliwa na tatizo la kupunguzwa kwa mishahara na marupurupu yao. Vikosi hivyo vinalalamika kuwa wanasiasa wanavilenga.

Police Captain Robert Gardner spricht durch ein Megafon zu den Demonstranten The following information applies for all pictures Tags Occupy Wall Street, Stop and Frisk, New York, Brownsville, Protest Name of the photographer Jonah Engle When was the pic taken? November 1, 2011 Where was the pic taken Brownsville, Brooklyn, NY Series Title: Pictures of a demonstration, in Brownsville, Brooklyn, against the New York Police Department’s stop and frisk policy. For all pictures: Rechteeinräumung: I hereby declare that I took this pic and giving DW the right to use it online.

Polisi wa New York

Mfamasia Michael Nastro alifurahishwa sana na jinsi polisi walivyopambana na jambazi mmoja katika eneo la jirani na kwake mwaka uliopita. Jambazi huyo aliyekuwa na bunduki aliingia katika duka moja la madawa na kuwaua watu wanne huku akibeba pia madawa. Polisi wa eneo hilo waliongeza shughuli za doria na kuwaelimisha wakaazi kuhusu nini cha kufanya endapo tukio kama hilo litafanyika tena. Jambazi huyo alishikwa baada ya siku tatu tu.

Lakini Nastro, mwenye miaka 50, anasikitika sana kuhusu malipo ya polisi na marupurupu yao. Anayo mawazo yanayopingana kwa sababu anataka kuhudumiwa vizuri na polisi, lakini pia ni mlipa kodi. Kwake ni lazima kuwe na usawa kati ya hizo mbili.

Italian firefighters carry the body of a worker who died in a factory collapse in Medolla, Italy, Wednesday, May 30, 2012. A magnitude 5.8 earthquake struck Tuesday that felled old buildings as well as new factories and warehouses in a swath of Italy north of Bologna. The quake, which followed a May 20 magnitude-6.0 quake in the same area, dealt another blow to one of the country's most productive regions at a time when Italy is struggling to restart its economy. (Foto:Gregorio Borgia/AP/dapd)

vikosi vya wazimaji moto.

Kwa kawaida wananchi wa Marekani wamekuwa wakiunga mkono swala la kuongezwa kwa mishahara na marupurupu ya polisi na wazima moto ambao katika kazi zao huhatarisha maisha yao, ilimradi kuhakikisha usalama wa wananchi. Walizidi hata kuunga mkono swala hilo hasa baada ya kifo cha wafanyakazi wa dharura wengi katika mashambulio ya Kituo cha kimataifa cha Biashara jijini New York mnamo September tarehe 11 mwaka 2011.

Lakini hali ya uchumi inapoendelea kuzorota na serikali za mitaa kukumbwa na matatizo makubwa katika hazina za fedha, mtazamo huo unabadilika. Tangu kuanza kuzorota kwa uchumi mwaka 2007, miji mingi mikubwa imeanza kupunguza mishahara na marupurupu .

Katika miji ya San Diego, mji wa pili kwa ukubwa California, ikifuatwa na San Jose, watu walipiga kura kwa wingi ili kuondoa marekebisho ya marupurupu. Katika mji wa San Diego wafanya kazi wote sasa watatakiwa kuchagua kati ya kupunguzwa kwa marupurupu yao ama kuongezwa kwa ada ya malipo ya mafao.

Kwengineko Stockton na San Bernardino, watumishi wa serikali wanasema bei ya usalama ndio imesababisha kwa asilimia kubwa miji mawili kufilisika. Katika mji wa Vallejo, San Francisco, ambao ilikuwa mji wa kikosi cha wanamaji cha Marekani, malipo ya usalama na marupurupu yalichukua robo tatu ya bajeti ya jiji hilo.

Jiji la Detroit linakumbwa na uhalifu mwingi zaidi katika nchi, lakini ilishusha malipo na marupurupu ya afya kwa wafanya kazi wa jiji hilo, wakiwemo polisi kwa asilimia 10, uamuzi ambao meya wa mji huo anasema utalisaidia jiji hilo kuokoa dola milioni 102 kila mwaka. Juhudi za Muungano wa maafisa wa polisi wa Detroit kuupinga uamuzi huo kortini zilishindikana , rais wa muungano huo akiwa analalamika kuhusu jinsi uamuzi huo utaathiri uwezo wa Detroit kuwaandika polisi wengine.

Kupata usawa kati ya uwekaji akiba na usalama ni kazi ngumu sana. Imekuwa kawaida kwa wapigaji kura kuunga mkono kupunguzwa kwa mishahara ya walimu na wafanya kazi wengine wa umma, lakini polisi na wazima moto wamekuwa wakiponea. Aidha sasa wanasiasa wameanza kuwalenga polisi na wazima moto.

Jim Carver ni rais wa Muungano wa kihisani wa polisi katika jimbo la Nassau. Alikiambia kituo cha habari la Reuters kuwa baada ya mashambulio ya tarehe 11 September mwaka 2011, hakukuwa na mwanasiasa ambaye hangemkumbatia polisi ama mzima moto. Miaka 10 au 12 baadaye wamekuwa wa wakulaumu kwa kila kitu. Wamekuwa kama maadui. Kwa maoni yake hawakumlazimisha kuongezwa mishahara na marupurupu , mikataba hiyo ilijadiliwa kwa haki.

Mwandishi: Trizer Ochieng
Mhariri: Miraji Othman

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com