1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Poland: Urusi ijieleze baada ya kombora kukiuka usalama wake

Lilian Mtono
24 Machi 2024

Poland imeitaka Urusi kutoa maelezo baada ya makombora ya Urusi yaliyofyatuliwa kuelekea miji ya magharibi mwa Ukraine kukiuka usalama wa anga nchini humo.

https://p.dw.com/p/4e4WX
Warsaw, Poland 2023 | Mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Kitaifa baada ya ukiukaji wa usalama wa anga
Waziri wa Ulinzi wa Poland Wladyslaw Kosiniak-Kamysz amesema Poland imewasha mitambo ya kujilinda baada ya kombora la Urusi kuvuka mpaka wake wa anga Picha: Dawid Zuchowicz/Agencja Wyborcza/REUTERS

Kulingana na Poland, kombora hilo lililokuwa likisafiri kwa kasi ya kilomita 800 kwa saa karibu mita 400 kutoka ardhini, lilivuka karibu kilomita mbili juu ya mpaka wa Poland.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Poland Apwel Wronski amesema kwenye taarifa yake kwamba, pamoja na mengineyo, wanalitaka Shirikisho la Urusi kumaliza mashambulizi ya kigaidi dhidi ya watu wa Ukraine, kuvimaliza vita na kujikita kwenye matatizo yake ya ndani.

Waziri wa Ulinzi wa Poland Wladyslaw Kosiniak-Kamysz amesema, kufuatia mashambulizi hayo, Poland imewasha "mifumo yote ya ulinzi wa anga na ya jeshi la anga".