1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS.UNICEF yalalamikia kuajiriwa wanajeshi watoto

5 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUm

Mkutano wa shirika la umoja wa mataifa la watoto UNICEF umeanza mjini Paris Ufaransa.

Mkutano huo unaangazia hatma ya takriban watoto 250,000 ambao wameorodheshwa katika makundi ya kijeshi.

Kiasi cha nchi kumi na mbili zinatuhumiwa na umoja wa mataifa kwa kuendeleza harakati za kuwaajiri wanajeshi watoto.

Watayarishi wa mkutano huo wanataraji kuwa nchi washiriki 60 katika mkutano huo pamoja na makundi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yataweza kuafikiana njia muafaka zitakazowezesha sheria ya kuzuia kuajiriwa watoto katika huduma za kijeshi na wakati huohuo kuwatafutia watoto walioathirika njia mbadala za kurudi katika maisha ya kawaida.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Philippe Douste Blazy amesema kuwatumia watoto katika shughuli za kijeshi huwaacha watoto hao kuwa sawa na bomu lililotegwa na ambalo litalipuka wakati wowote maishani mwao.

Siku ya Jumapili jeshi la Uingereza lilikiri kuwa liliwapeleka wanajeshi 15 nchini Irak waliokuwa chini ya umri wa miaka 18 tangu mwaka 2003.