1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiVatican

Papa Francis aendesha misa ya Alhamisi akiwa imara

28 Machi 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo ameendesha misa ya Alhamis Kuu katika kanisa la Mtakatifu Petro akionekana kuwa imara kiafya.

https://p.dw.com/p/4eEHw
Papa Francis aongoza ibada ya Alhamisi Kuu akiwa imara kiafya
Papa Francis akiongoza moja ya ibada katika kanisa la Matakatifu Basilica huko Vatican Disemba 24, 2023. Picha: Gregorio Borgia/AP Photo/picture alliance

Papa Francis mwenye umri wa miaka 87 mara kadhaa amezongwa na maradhi yanayohusiana na kupumua katika kipindi hiki cha baridi na katika misa ya Jumapili ya Matawi iliyopita, alishindwa kusoma hotuba yake katika dakika ya mwisho.

Kiongozi huyo wa kidini ana siku kadhaa zijazo zenye shughuli chungunzima ambazo zitakuwa kama mtihani kwa afya yake.

Hapo kesho Ijumaa anatarajiwa kuongoza Njia ya Msalaba ya Ijumaa Kuu kisha Jumamosi jioni, aongoze misa ya maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka.

Jumapili atafanya misa nyengine ya Pasaka itakayofuatwa na hotuba yake itakayoangazia majanga na mizozo inayoikumba dunia na binadamu.