1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa wa zamani adai kuna wanaotaka kumnyamazisha

4 Mei 2020

Kiongozi wa zamani wa kanisa Katoliki, Papa mstaafu Benedikti wa 16 amewatuhumu wapinzani wake kutaka kumyamazisha wakati akishambulia ndoa za jinsia, kupitia kitabu kipya kilichoidhinishwa kuhusu maisha yake.

https://p.dw.com/p/3bkl4
Vatikan l Der emeritierte Papst Benedikt XVI besucht Papst Franziskus
Picha: Getty Images/J. Simon

Katika kitabu hicho kilichochapishwa leo nchini Ujerumani, Papa huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 93 ambaye jina lake la kuzaliwa ni Joseph Ratzinger amedai kwamba katika maisha yake kama Benedikti wa 16 alikuwa muhanga wa upotoshaji wa makusudi wa hali halisi, katika hatua alizochukuwa kuingilia kati katika mijadala ya imani ya kanisa.

Hayo yamebainishwa katika vipengee vya kitabu hicho vilivyochapishwa na vyombo vya habari Ujerumani na shirika la habari la DPA. Inaelezwa kwamba kiongozi huyo wa zamani wa kanisa katoliki duniani Benedikti wa 16 amesema yu radhi kutoweka wazi sababu haswa, kwa nini watu wanataka kuinyamazisha sauti yake.

Kanisa Katoliki nchini Ujerumani kwa miaka limekuwa likiongozwa na viongozi wa dini hiyo wanaotaka zaidi mageuzi kuliko misimamo mikali ya utamaduni wa kanisa unaofungamanishwa na Ratzinger.