Imani
Papa Leo akosoa ukosefu wa usawa barani Afrika
22 Aprili 2026
Matangazo
Ameyasema hayo katika Misa Takatifu aliyoiongoza mjini Mongomo ambapo amezungumzia pia ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo na kuwaombea heri watu wa nchi hiyo.
Waafrika waaswa kulinda heshima na utu
Katika misa hiyo amenukuliwa akisema kuwa, "Nawaombea uhuru uongezeka na heshima ya mtu ilindwe siku zote. Ninawafikiria masikini na familia zinazopitia magumu. Ninawakumbuka wafungwa ambao mara nyingi wanalazimika kuishi kwenye mazingira magumu ya usafi na afya."
Baada ya misa hiyo Papa Leo alielekea kulitembelea gereza maarufu katika mji wa Bata ili kuwapa matumaini wafungwa na kuwakumbusha kuwa kanisa liko pamoja nao.