1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis awarai vijana wa Kongo kupiga vita rushwa

2 Februari 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema anawategemea vijana kuiongoza Afrika kwenye mustakabali bora bila vita, mateso na rushwa.

https://p.dw.com/p/4N26r
DR Kongo | Papst Franziskus in Kinshasa
Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema anawategemea vijana kuiongoza Afrika kwenye mustakabali bora bila vita, mateso na rushwa.

Katika mkutano wake na waumini wapatao 65,000 kwenye uwanja wa mpira mjini Kinshasa, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani amewahimiza watu wa Kongo kutokubali kulaghaiwa na watu au makundi yanayojaribu kuibakisha nchi yao katika vurugu na ukosefu wa utulivu, ili waendelee kuidhibiti bila kuwajibika kwa yeyote.

Papa Francis anaizuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wiki hiki na atakwenda Sudan Kusini kesho Ijumaa. Mataifa hayo mawili yamekumbwa tena na mizozo ya umwagaji damu, ambapo vurugu zikiongezeka hasa mashariki mwa Kongo.