1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Pakistan: Adhabu ya Imran Khan yasimamishwa

29 Agosti 2023

Mahakama kuu ya nchini Pakistan, imesimamisha hukumu iliyotolewa hivi karibuni kwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Imran Khan.

https://p.dw.com/p/4VhHw
Mawakili wasema Khan amepewa dhamana, lakini wanahofia anaweza kukamatwa tena.
Mawakili wasema Khan amepewa dhamana, lakini wanahofia anaweza kukamatwa tena.Picha: Mohsin Raza/REUTERS

Waziri huyo wa zamani wa Pakistan amekuwa jela tangu alipohukumiwa mapema mwezi huu baada ya kukutwa na hatia ya kuuza zawadi za nchi kinyume cha sheria wakati alipokuwamo madarakani kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka uliopita.

Kutokana na hukumu hiyo tume ya uchaguzi ilimpiga marufuku kugombea katika uchaguzi kwa muda wa miaka mitano.

Mawakili wake walisema Khan amepewa dhamana, lakini wanahofia anaweza kukamatwa tena kuhusiana na kesi mojawapo kati ya zaidi ya madai 200 yaliyotolewa dhidi yake tangu alipoondoka madarakani mwezi Aprili mwaka uliopita.