Orodha ya vipindi vyetu | Redio | DW | 14.07.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Redio

Orodha ya vipindi vyetu

Kwa habari motomoto, makala na uchambuzi DW huwapa fursa wasikilizaji kuufahamu ulimwengu- siasa, haki za binadamu, mazingira, wanawake, vijana, afya, utamaduni na ulimwengu wa Vijana. Masaa matatu kwa siku.

Habari za Ulimwengu: Taarifa ya habari mpya juu ya matukio ya hivi karibuni duniani kote- mara tatu kwa siku, na sehemu maalum ya Habari za Afrika matangazo ya Mchana na jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

Dunia Yetu Leo Asubuhi/ Mchana/ Jioni: Uchambuzi wa taarifa za ulimwengu, mahojiano, na ripoti za waandishi wetu sambamba na maoni ya wasikilizaji na marafiki zetu kwenye kurasa za kjamii na simu.

Afrika kwa kina

Habari za Afrika: Taarifa ya habari juu ya matukio ya hivi karibuni kote barani Afrika.

Afrika Wiki Hii: Uchambuzi wa matukio yaliyojiri barani Afrika iwe kwenye masuala ya kisiasa, kijamii, kiuchumi au kiutamaduni unaompa msikilizaji muhtasari wa namna bara hilo lilivyokuwa kwa juma nzima.

Kinagaubaga: Mahojiano ya moja kwa moja ya kila wiki na masuali magumu kwa mmoja wa watu muhimu kuhusu jambo muhimu lililotokea katika mataifa ya Afrika ya Mashariki na Kati.

Afrika Magazetini: Ripoti za magazeti ya Ujerumani zilizoaliangazia bara la Afrika kwa kipindi cha wiki moja, mada zilizopewa umuhimu na maoni ya wahariri wa Ujerumani kuhusu yanayojirini barani humo.

Makala za kila wiki

Maoni: Mjadala unaowashirikisha wataalamu, wachambuzi, wanasiasa, wakijalidili masuala ya kimataifa na kikanda, kujenga uwelewa wa wasikilizaji juu ya masuala yanayogusa maisha yao katika nyanja zote.

Mbiu ya Mnyonge: Makala inayoangazia wapi na vipi haki za binaadamu zinavunjwa barani Afika na ulimwenguni kwa ujumla na namna mashirika ya haki za binaadamu yanavyozipigania.

Mazingira: Makala inayozungumzia ulinzi wa mazingira duniani, tabia nchi, matumizi ya madawa yanayochafua mazingira na yanayohusika nayo kwa lengo la kutoa elimu ya kuyalinda mazingira.

Afya: Makala inayozungumzia aina mbalimbali za maradhi, njia za kujikinga na matibabu, usafi, na ushauri wa kuwa na afya bora.

Michezo: Yanayojiri katika nyanja ya michezo, kuanzia ligi za soka Afrika Mashariki na Kati hadi makombe ya Ulaya, Asia, Marekani na duniani, mpira wa kikapu, riadha, mashindano ya mbio za magari, tennis na kriketi.

Wanawake na Maendeleo: Changamoto wanazokabiliana nazo wanawake kwenye jamii, taswira za wanawake madhubuti ambao ni kigezo bora kwa wenzao na namna wanavyoziendeleza familia zao.

Sura ya Ujerumani: Makala inayoonesha namna Wajerumani wanavyoishi, jinsi demokrasia yake inavyofanya kazi na taswira mbalimbali za kitamaduni, kisiasa na kiuchumi zinaoifanya Ujerumani kuwa Ujerumani.

Makala Yetu Leo: Makala inayoangazia masuala muhimu ya Afrika na hasa Afrika Mashariki na Kati, kama vile kilimo, fedha, uchumi na siasa, vita dhidi ya uhalifu, ufisadi ama ujenzi wa utawala bora.

Mwangaza wa Ulaya: Matukio muhimu ya barani Ulaya, mahusiano kati ya Ulaya na Afrika, namna Umoja wa Ulaya unavyoshughulikia masuala mbalimbali kama uhamiaji, na pia mtazamo wa maisha ya kila siku barani humo.

Ulimwengu wa Vijana

Sema Uvume: Vijana na mitandao ya kijamii, wanachokizungumzia, App mpya, usalama kwenye mitandao, hatari iliyomo, mafunzo kupitia ulimwengu wa mitandao na yote kuhusu teknolojia ya habari na mawasiliano.

Vijana Mchaka Mchaka: Wakati wa vijana kuonesha staili na fasheni zao, mambo mapya na mitindo ya maisha wanayoishi mitaani na vijiweni na namna zinavyomaanisha kwenye maisha yao ya ujana.

Vijana Tugutuke: Kila wiki, vijana hujadiliana na waandishi wetu kote Afrika Mashariki juu ya masuala yanayotokea sasa.

Noa Bongo, Jenga Maisha Yako: Kipindi murua kabisa cha kuwaelimisha vijana kupitia tungo za waandishi wa Kiafrika kuhusu mambo yanayowagusa vijana. Michezo yake huigizwa na wachezaji vijana nchini Tanzania

Burudani

.Jukwaa la Manufaa: Kipindi kinachopaisha sauti ya msikilizaji moja kwa moja kuelezea yake ya moyoni na wahusika wengine, hasa viongozi wa kitaifa na kimataifa, wakisikie kutoka kwake.

Utamaduni na sanaa: Kuuangazia kwa karibu utamaduni- kuanzia tamasha la Busara visiwani Zanzibar hadi maonyesho ya Berlinale nchini Ujerumani.

Karibuni: Wasaa wa burudani pamoja na wageni wetu wa kila wiki, uchambuzi wa lugha kupitia Kiswahili Kina Wenyewe, ushairi na hadithi fupi kumfanya msikilizaji apate ladha nyengine nje ya habari.

Umeipata Hiyo: Dondoo za masuala ya kushangaza na kufurahisha yanayotokea duniani, ambayo huleta ucheshi na pia mafunzo kwa jamii.

Salamu: Muda wa kusalimiana, kutakiana kheri na kufurahi pamoja kupitia salamu na muziki.