1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

OPCW yapokea tuzo ya amani ya Nobel

Mjahida11 Oktoba 2013

Tuzo ya amani ya Nobel mwaka wa 2013 imeliendea shirika la kimataifa la kudhibiti silaha za kemikali OPCW, kutokana na juhudi zake kubwa za kuangamiza silaha za sumu.

https://p.dw.com/p/19xyu
Jengo la OPCW lililoko mjini The Hague Uholanzi
Jengo la OPCW lililoko mjini The Hague UholanziPicha: picture-alliance/dpa

Kulingana na mwenyekiti wa Kamati ya Norway ya Nobel Thorbjoern Jagland, wametoa tuzo kwa shirika hilo kutokana na namna inavyoshughulikia uangamizi wa silaha hatari za nyuklia.

Shirika hilo lililoundwa mwaka wa 1997 lilitwikwa jukumu la kuondoa na kuangamiza kabisa silaha za sumu duniani kote. Tuzo hiyo ambayo inajumuisha zawadi nono ya kitita cha dola milioni 1.25 ilitangazwa muda mfupi uliopita mjini Oslo Norway.

Baadaye Disemba 10 shirika hilo linatarajiwa kukabidhiwa rasmi tuzo hiyo huko huko mjini Oslo ambako pia itakuwa ni siku aliyofariki muanzilishi wa tuzo hiyo, Alfred Nobel. Tuzo ya amani ya Nobel imekuwa ikitolewa tangu mwaka wa 1985.

Kulingana na msemaji wa OPCW Michael Luhan, tangu shirika hilo lilipoundwa miaka 16 iliopita limeharibu takriban tani 57,000 za kemikali ya nyuklia, nyingi zikiwa zile zilizoachwa katika vita baridi vya Marekani na Urusi.

Viongozi wa shirika la OPCW
Viongozi wa shirika la OPCWPicha: Reuters

Shirika hilo lenya wanachama nchi 189 na lililo na makao yake makuu mjini The Hague, Uholanzi, lina takriban wafanyakazi 500.

Umuhimu wa shirika hilo ulionekana zaidi mwaka huu baada ya gesi yenye sumu ya Sarin kutumika mjini Damascus mwezi Agosti na kusababisha mauaji ya takriban watu 1,400.

Marekani moja kwa moja ilimshutumu rais wa Syria, Bashar Al Assad, kwa kutumia silaha hizo, shutuma ambazo alikazinusha vikali na kusema waasi ndio waliotumia gesi ya sumu dhidi ya raia wa Syria.

OPCW yasema Syria yatoa ushirikiano mkubwa

Baada ya Assad kukumbwa na vitisho kutoka Marekani kwamba huenda nchi hiyo ikaingilia kijeshi kutokana na matumizi ya silaha hizo, Assad alikubali kuharibu silaha zake zote za Nyuklia na kutoa fursa kwa wataalamu wa shirika la OPCW kuingia nchini humo na kutekeleza majukumu yao.

Hata hivyo shirika la OPCW, linasema Syria imeamua kutoa ushirikiano na huenda silaha za kemikali za nchi hiyo zikaangamizwa katikati ya mwaka 2014.

Wataalamu wa OPCW nchini Syria
Wataalamu wa OPCW nchini SyriaPicha: picture-alliance/dpa

Hata hivyo, Hamish De Bretton, mtaalamu wa maswala ya Nyuklia anasema shirika hilo limestahili kupokea tuzo hiyo lakini linakabiliwa na changamoto kubwa.

"Hii ni tuzo nzuri kabisa kwa shirika la OPCW lakini kutokana nan kile kitakachoonekana nchini Syria kwa mwezi ujao ama siku chache zijazo nmi muhimu sana na bila kupata uungwaji mkono wa upinzani nadhani itakuwa jukumu lililo na changamoto kubwa," Alisema Hamish de Bretton.

Kwa miaka miwili mfululizo tizo ya amani ya Nobel imetuzwa kwa mashirika, mwaka uliopita shirika la Umoja wa Ulaya lilivikwa taji hiyo ya tuzo ya amani ya Nobel.

Mwandishi: Amina Abubakar/Reuters/AP

Mhariri: Josephat Charo