Olimpik Beijing imefunguliwa | Michezo | DW | 08.08.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Olimpik Beijing imefunguliwa

Michezo ya 29 ya olimpik imefunguliwa rasmi leo 8-08-08.

Bach,Rais wa kamati ya olimpik ya Ujerumani .

Bach,Rais wa kamati ya olimpik ya Ujerumani .

Kama mlivyosikia michezo ya 29 ya olimpik ya Beijing 2008,imefunguliwa rasmi hivi punde na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Hu Jintao akiwa pamoja na Rais wa Halmashauri Kuu ya Olimpik ulimwenguni Jacques Rogge.

Kabla kuitangaza michezo hiyo rasmi imefunguliwa,kulifanyika tafrija mbali mbali katika Uwanja mkuu wa Olimpik uliosheheni watazamaji 90,000 .jumla ya viongozi wa dola 80 pamoja nao Rais George Bush wa Marekani,Sarkozy wa Ufaransa,waziri mkuu Putin wa Russia hadi Kufour wa Ghana,Oumar Bongo wa Gabun ,Eduardo Dos Santos wa Angola na Nkurunziz wa Burundi walikuwapo uwanjani.

►◄

Sherehe ya ufunguzi za masaa 3 na nusu iliongozwa na mkurugenzi wa filamu Zhang Yimou,iliwafungulia pazia wanariadha 5000 kutoka mataifa 204 waliocalia mavazi ya kitaifa ya urembo na maridadi ajabu kama yale ya waburundi na Rwanda,Ghana na Mali,Kongo mbili hadi st.kitis,huko Karibik.Wanariadha pia wa Kenya,Uganda na Malawi na Tanzania waliteremka uwanjani kwa mfumo mpya usio wa mwanzo wa herufi ya jina la nchi zao.mara wakifuata maandishi ya kichina.

Umati wa mashabiki 90,000 uwanjani na mabilioni ulimwenguni umejionea fashfash 35,000 zikipaa angani :

Katika nchi ambako 8 ni nambari ya bahati, bendera ya taifa ya china ilibebwa uwanjani saa 2 na dakika 8,tarehe 8 leo mwaka 2008.

Waliandaa michezo hii wakitamani sana kuangukiwa na bahati njema.Bahati ya kubariki mafanikio makubwa ya kuibuka China dola kuu la kiuchumi mara nyingi likigubikwa na wingu la mashtaka ya kukanyaga haki za binadamu,uhuru wa vyombo vya habari na machafuko huko Tibet na katika kambi ya magharibi juu ya sera zake za kigeni kama kuelekea Dafur.

Viongozi wengi wa dola wamehudhuria ufunguzi huu na wengine kama Kanzela wa Ujerumani Angela Merkel, wamejiweka kando wengine kulalamika juu ya kukiukwa haki za binadamu na wengine kwa udhuru mwengine.

Kabla ya kuwasili uwanjani na mkewe Laura, rais Bush akiwa nchi jirani ya Thailand, Rais Bush alielezea wasi wasi wake mkubwa juu ya upungufu wa uhuru wa kuabudi na kukanyagwa haki za binadamu nchini china.

Zaidi ya askari laki 1 wanashika zamu katika michezo hii huku pakitoka maonyo kila mara ya hatari ya mashambulio hasa kutoka kikundi cha kigaidi cha kiislamu kinachogombea kujitenga huko Sikjiang.

Barabara za mji wa Beijing unaokaliwa na wakaazi milioni 17 alaasiri ya leo kinyume na kawaida, zilikuwa tupu.Wakaazi wake wengi wakiwa majumbani baada ya serikali kuitangaza siku ya leo ni ya mapumziko.

Swali nani angewasha mwenge wa olimpik uwanjani, iliwekwa siri kubwa na uvimu kwamba stadi maarufu wa China Yao ming aliebeba mwenge mjini Beijing,haukuthibitishwa.

Pale mwishoe, rais Hu Jintao alipotzangaza michezo ya 29 ya kisasa ya olimpik imefunguliwa rasmi,wanariadha wake kwa waume walifunguliwa mlango wa kinyan'ganyiro cha medali za dhahabu,fedha na shaba kuanzia kesho hadi August 24.