Olimpik Beijing 2-08-08 imewadia. | Michezo | DW | 07.08.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Olimpik Beijing 2-08-08 imewadia.

Michezo ya Olimpik ya beijing inafunguliwa rasmi leo 2-08-08.

Rais Hu jintao na mgeni wake katika olimpik-George Bush.

Rais Hu jintao na mgeni wake katika olimpik-George Bush.

Tarehe 8-08-2008 iliosubiriwa kwa hamu kuu imewadia:Michezo ya 29 ya olimpik ya Beijing-ya tatu barani Asia baada ya ile ya Tokyo, 1960 na Seoul,1988.Swali linaloulizwa hivi sasa: jinsi gani hali ya hewa itakavyokua leo,kwani sherehe na fashfash zilizopangwa zitategemea hali ya hewa.Je, itanyesha mvua na vipi ukungu utaondoka na hewa safi itatanda ?

Na je, sherehe za leo za ufunguzi zitapita bila ya malalamiko ya kisiasa yalioandamana na mwenge wa olimpik tangu ulipoanza safari yake huku Ulaya hadi kuwasili siku 2 zilizopita mjini Beijing? .

Ramadhan ali anawafungulia pazia la sherehe za leo za ufunguzi wa michezo ya Beijing, 2008.

►◄

Ufunguzi wa michezo ya olimpik hii leo ni kilele cha maandalio ya kiasi ya miaka 7 na masaa machache kutoka sasa,rais wa halmashauri kuu ya Olimpik Ulimwenguni,mbelgiji Jacques Rogge, ataitangaza michezo ya 29 ya kisasa ya olimpik imefunguliwa.

Kuanzia hapo bunduki zitalia kuanzisha mashindano ya kunyan'ganyia medali za dhahabu,fedha na shaba katika jumla ya michezo 28.

Jana mshindo mkubwa ulisikika huko Tianjin,pale wenyeji China walipotia bao lao la kwanza kuipa ushindi timu yao ya wasichana ya dimba dhidi ya sweden wa mabao 2:1.Shangwe zilisikika za "China songa mbele".

China imeshinda kwahivyo mechi yake ya kwanza ya michezo ya 29 ya olimpik na leo imeuahidi ulimwengu wa Olimpik mjini Beijing, shangwe na shamra shamra.Jogoo wa basketball YAO Ming ataongoza leo mlolongo wa wanariadha wa China akipepea bendera yao uwanjani Beijing. uwanjani na kuiongoza pia China katika basketball.

Michezo ya Beijing imekumbwa na malalamiko ya kisiasa ambayo China inatumai baada ya ufunguzi wa leo itasahauliwa na macho ya mashabiki yatakodolewa nani amenyakua medali za dhahabu,fedha na shaba.

rais wa Halmashauri kuu ya olimpik ulimwenguni,mbelgiji Jacques Rogge, binafsi alieshiriki mara tatu katika olimpik katika mashindano ya mashua anasisimkwa kabla ya ufunguzi wa leo.

Rogge anatumai hakutazuka fujo la malalamiko ya kisiasa au hujuma yoyote.Anakumbusha kuwa wanariadha wanatakiwa kuheshimu kanuni ya 51 ya Olimpik.Yaani hawaruhusiwi kufanya propaganda tangu za kisiasa,za kidini au za kibiashara au hata maandamano.Wanapaswa pia kuheshimu sheria za China .Jacques Rogge anatumai michezo hii itaifungulia China mlango wa kujianika ulimwenguni.Kwani, china ni dola lenye historia ya miaka 5,000.

Waandazi wa Beijing wamearifu kuwa zaidi ya wanariadha 11,000 wataania medali 302 katika michezo 28 mbali mbali-riadha ambao ni uwanja wa waafrika ndio moyo na msisimko wa olimpik ulipo.Ni hapa tunatazamia wanariadha wa Kenya na Ethiopia kutamba na kupepea bendera ya Afrika kuanzia mita 800 hadi mbio za marathon.

Kinachovutia mara hii, tangu kikosi cha wanaume hata kile cha kike ni imara kupepea bendera za Afrika.

Changamoto ya kuamua nani mwanadamu wa kasi kabisa itakua kati ya wamarekani na wajamaica: Tyson Gay bingwa wa dunia kutoka Marekani atakumbana na changamoto kali kutoka bingwa rekodi ya dunia,mjamica Usain bolt alitangaza kukimbia masafa yote 2-mita 100 na mita 200.

Halafu kuna bingwa wa zamani wa rekodi ya dunia pia kutoka Jamaica Asafa Powel aliekuja hivi punde kwa meno ya juu.

matumaini ya wenyeji China katika medani ya riadha yananin'ginizwa kwa bingwa wao wa olimpik wa Athens, 2004 Liu Xiang.China lakini inahofia hapo kuwa bingwa mpya wa rekodi ya dunia Dayron Robles hatawatilia kitumbua chao mchanga.