1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Deutschland Bundestag | Vereidigung Olaf Scholz
Picha: Ina Fassbender/AFP/Getty Images

Olaf Scholz aapishwa kuwa Kansela wa Ujerumani

Amina Mjahid
8 Desemba 2021

Serikali mpya ya muungano nchini Ujerumani ikiongozwa na Olaf Scholz wa chama cha Social Democratic - SPD imeapishwa kuchukua usukani mjini Berlin.

https://p.dw.com/p/4409g

Hatua hiyo imehitimisha muhula wa miaka 16 wa kansela anayeondoka Angela Merkel kwenye uongozi wa taifa hilo kubwa zaidi kiuchumi barani Ulaya.

Baada ya kupigiwa kura bungeni, Scholz alielekea kwenye kasri la rais, ambako Rais Frank-Walter Steinmeier alimteuwa rasmi kuwa kansela, kisha akarejea bungeni kuapishwa. 

soma zaidi: Olaf Scholz aidhinishwa kuwa Kansela wa Ujerumani

Mawaziri 16 wa serikali mpya pia wamepitia mchakato huo huo. Scholz anatarajiwa kusafiri kwenda Ufaransa na Ubelgiji katika ziara yake ya kwanza ya kigeni baada ya kuingia madarakani.

Atafanya mazungumzo na Rais Emmanuel Macron mjini Paris kabla ya kukutana na Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel katika maandalizi ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya wiki ijayo.

Kansela Scholz pia atakutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg Ijumaa jioni. 

Uchambuzi: Je, ni masuala yapi Olaf SCholz anapaswa kutilia maanani?