1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Okonjo-Iweala aonya athari za vita, ukosefu wa utulivu

Tatu Karema
26 Februari 2024

Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Ngozi Okonjo-Iweala, ameonya kuwa vita, hali ya kutotabirika na ukosefu wa utulivu vinadhoofisha uchumi wa dunia.

https://p.dw.com/p/4csnH
Ngozi Okonjo-Iweala wa WTO.
Mkuu wa Shirika la Biashara la Ulimwengu (WTO), Ngozi Okonjo-Iweala.Picha: Li Xin/dpa/picture alliance

Okonjo-Iweala alisema shirika lake linapaswa kuzingatia mageuzi wakati mataifa mengi yanapofanya chaguzi ambazo zinaweza kuleta changamoto mpya.

Okonjo-Iweala alilipongeza shirika hilo wakati linapofanya mkutano wake wa kila baada ya miaka miwili katika Umoja wa Falme za Kiarabu, likiwa linakabiliwa na shinikizo kutoka Marekani na mataifa mengine.

Soma zaidi: Ngozi Okonjo-Iweala mwanamke aliyeleta fahari Afrika

Lakini alielezea kwa uwazi kuhusu jinsi athari za ongezeko la bei ya chakula, nishati na mahitaji mengine muhimu zinavvochochea kuwepo kwa mazingira tata ya kisiasa.

Wakati wa mkutano huo wa wiki hii mjini Abu Dhabi, mataifa 164 wanachama wa WTO yatajadili makubaliano ya kupiga marufuku ruzuku inayochangia uvuvi kupita kiasi, kuongeza muda wa kusitisha ushuru kwenye vyombo vya habari vya kidijitali kama vile filamu na michezo ya vidio na masuala ya kilimo.